Katika biblia Mungu
anaonekana kutumia alama nyingi na ishara mbali mbali ili kufikisha ujumbe Fulani
kwa watu wake,Mfano katika Mwanzo 9:12-16 Mungu anatumia upinde wa mvua kama
agano lake na Nuhu kuwa hataiangamiza Nchi tena kwa maji,Mungu alitumia mkate
kama ishara au kieleleza cha uwepo wake na watu wake (hesabu 4:7).
Namba saba ni
moja ya namba za muhimu sana kwenye biblia takatifu.Ni namba ambayo imetajwa
zaidi katika neno takatifu la Mungu,Namba hii inatajwa mara 735 ambayo pia
inagawanyika kwa saba na kupata 105.
Matumizi ya
kwanza ya namba 7 yanaonekana katika wiki ya uumbaji katika Mwanzo 1.Mungu
alitumia siku 6 kuumba mbingu na Nchi na kupumzika katika siku ya 7. Siku hii
ya saba ilitengwa kama siku ya pekee kwa wana wa Israeli kama siku ya sabato na
kupumzika. (Kumbukumbu la torati 5:12).
Sasa tangu
mwanzo wa uumbaji,namba saba inaonekana ikiwakilisha ukamilifu au utimilifu Fulani
(completeness or divine perfection).kutoka hapo unaanza kuona jinsi namba saba
inavyousishwa katika ukamilifu kaika vifungu mbali mbali vya neno la
Mungu.MFANO
Mungu aliamuru
kuwa wanyama wanaotakiwa kutolewa sadaka inabidi wawe na siku 7 na kuendelea
(kutoka 22:30),Naamani anaambiwa na nabii kuwa akajichovye mara 7 kwenye maji ya mto yordani ili akamilishe usafishwaji wake na apone ukoma (2wafalme 5:10) na
amri ambayo alipewa Joshua kuzunguka ukuta wa yeriko mara 7 ili uanguke.
Katika kitabu
cha ufunuo wa yohana tunaweza kuona MAKANISA 7,ROHO SABA,NYOTA SABA,MIHURI
SABA,TARUMBETA SABA,NYOTA SABA,WAFALME SABA Hii namba saba ilikuwa inaonyesha
ukamilisho wa kiroho au spiritual perfection.Maisha yote ya duniani yanategemea
namba saba.
Neno la Mungu
lote lipo kwenye namba saba (walawi 23:15-16) Namba saba na sabato katika
mistari hii yameunganishwa na neno ukamilisho au completeness.Neno ‘kutimia’
limeambatana na neno ‘sabato saba’. Baada ya siku ya saba kuisha inaonekana
kuna kitu kipya kilifuata hapa.
Pia neno ‘kutimizwa’
limeungana na neno ‘malaika saba’ kwenye Ufunuo 10:7.
Neno ‘kuumba’
limetumika mara saba kwenye uumbaji wa mungu (Mwanzo 1:1,1:21,1:27-hapaa
limetumika mara 3 halafu mwanzo 2:3 na 2:4). Mungu ameumba siku saba katika
wiki,hamna hata siku moja ambayo tulishawahi jiuliza kwann kuna siku saba
kwenye wiki,hizi siku ndio zinazoleta miaka na misimu mipya duniani.
Kuna note saba
za muziki duniani kote,muziki wote unaundwa kutokana na note hizo,mtu akitumia
note nane basi huwa anarudi kwenye ya kwanza ‘do” (do re mi fa so rat i……do).
Siku saba baada
ya Nuhu kuingia kwenye safina,mvua ikaanza,pia soma walawi 16:14,8:31-36).Pia
kulikuwa na sikuku saba agano la kale kasome
walawi23:1-44).
Ngoja nikuoneshe
kitu cha kushangaza,maisha yana operate katika cycle ya saba saba.Mabadiliko
yanatokea katika mwili kila baada ya miaka saba,kuna mifupa saba
shingoni,mifupa saba usoni,mifupa saba kwenye ankle,matobo saba kichwani,uzazi
mwingi ni katika kipeo cha saba.Kuku anaatamia siku 21,njiwa wiki 2, zaidi ya
specie 129 za mamaalia uzazi wao upo kwnye kipeo cha saba akiwemo na mwanadamu miezi 9 ambazo ni sawa
na siku 280.Ukiendelea kusoma bado kuna vitu vingi sanna vyenye maana ya saba
hapo ndo utajua kuwa Mungu ni fundi na hakosei.
HIKI
KIMENISHANGAZA SANA.
Mwanadamu
aliumbwa na Mungu siku ya sita.katika baadhi ya maandiko yanahusisha namba sita
na mwanadamu kwa mfano,’Number of beast’ katika ufunuo 13:18 hii inaitwa namba
ya mwanadamu ‘666’.Kama namba ya Mungu ni 7 basi mwanadanu ni 6 na 6 siku zote
ni pungufu ya 7 ndo maana maandiko yanasema kuwa wote tumetenda dhambi na
kupungukiwa na utukufu wa Mungu (warumi 3:23),Mwanadamu sio Mungu kama ilivyo 6
sio 7.
Kwa
kumalizia,kuna muda mwingine namba saba inakuwa kama faraja kwetu,kwa mfano
ukisoma biblia ya kiingereza(kjv) yesu
anatumia neno I AM mara 7 kwenye injili ya yohana lakini pia muda mwingine
namba sab ina tuchallenge,kwa mfano yesu snasema samehe saba mara sabini na
sehemu ingine namba 7 ipo kama hukumu.ufunuo 16:1 na walawi 26:18
Mungu awabariki
sana
Post A Comment:
0 comments: