"Nimewapenda ninyi, asema BWANA. Lakini ninyi mwasema, Umetupendaje? Je! Esau siye ndugu yake Yakobo? Asema BWANA; ila nimempenda Yakobo; bali Esau nimemchukia na kuifanya milima yake kuwa ukiwa, na urithi wake nimewapa mbweha wa nyikani". MAL. 1:2‭-‬3

Maneno haya pia yanajirudia kwenye kitabu cha WARUMI 1:9-13 kama ifuatavyo...

"Wala si hivyo tu, lakini Rebeka naye, akiisha kuchukua mimba kwa mume mmoja, naye ni Isaka, baba yetu, (kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye), aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo. RUM. 9:10‭-‬12"

Baba yetu isaka alikuwa na watoto wawili,yaani Yakobo na essau. Lakini mistari hapo juu inatuonyesha kuwa Mungu alimpenda yakobo hata kabla hawajazaliea na kabla hawajafanya chochote kizuri ama kibaya...Mungu akasema mkubwa atamtumikia mdodo na esau ndiye aliyekuwa mkubwa.

Swali ..sasa kwanini Mungu anachukia mtu au anakuwa na chuki wakati yeye ni pendo?
1YOHANA 4:8

JIBU..

Tunaposoma biblia hasa kwenye mistari kama hii,lazima tuangalie muktadha au context ya vifungu.
Hapa tunaona nabii malaki na mtume paulo,wanatumia jina la ESAU kumaanisha watu wa Edomu ambao sio wacha Mungu na ni kizazi cha ESAU. Rebeka alikuwa na watoto wawili,Yakobo ambaye baadae Mungu akamfanya taifa teule yaani israel,na Esau ambaye alitengeneza taifa la wasiomjua Mungu yaani wadomu. kwahiyo sio kwamba Mungu alimchukia esau kama tunavyodhani,ila alikuwa hajamchagua na ndio maana maandiko yanasema Esau "edomu" ni mtu au taifa ambalo Mungu hakulichagua kiwa taifa lake takatifu na sio kwamba alimchukia.

ukisoma MWAZO 9:33 utaona jinsi Mungu alivyokuwa amewabariki waedomu kwa kila kitu. Baada ya kuona hayo basi tutambue kuwa Mungu kumpenda Yakobo na kumchukia Esau hakuhusiani kabisa na hisia za wanadamu za kupenda.
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

6 comments:

  1. Hii ni nzuri sana,Mungu awabariki sana ,kwa maono haya makubwa.

    ReplyDelete
  2. Mungu awabariki watumishi wa Mungu aliye juu, tuko pamoja

    ReplyDelete
  3. Ubarikiwe sana mtu wa Mungu

    ReplyDelete
  4. Ubarikiwe sana mtu wa Mungu

    ReplyDelete