*ANZA SIKU NA BWANA*
Pastor Myamba Ministries
 JUA CHANZO CHA TATIZO LAKO.

 Unapoenda hospitali unaumwa kabla hujapewa dawa ni lazima wajue chanzo cha tatizo lako ili wakupe dawa sahihi zinazoendana na tatizo lako, ukipata dawa zisizo zahihi huwezi pona ugonjwa wako.

 Katika ulimwengu wa roho pia ni vyema kujua chanzo cha tatizo lako ili uombe sawasawa na chanzo cha tatizo lako, japo wengi wamekuwa wakipenda maombi zaidi kuliko kujua chanzo cha tatizo, kwani kuna matatizo mengine hayahitaji maombi bali yanahitaji kubadili MFUMO wa maisha yako,

mfano mzuri ni huu, Yohana 5:14 Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; *usitende dhambi tena,* lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.

 Hapa anamaanisha chanzo cha tatizo lake kimetokana na dhambi iliyokuwepo ndani yake, hivyo uponyaji wake uko kwenye kubadili mfumo wa maisha yake, japo injili ya namna hii huwa haipendwi na wengi lakini ndio ile injili isiyogoshiwa.
Nini chanzo cha tatizo lako?
Ni mhimu sana kujua ili kuwa na tiba yakudumu. Usikimbilie kunywa dawa, tafuta shida ni nini ili unywe dawa sahihi na upate uponyaji wakudumu. Uchumi wako unaanguka kila siku, hupandishwi cheo, mtaji unapotea kila siku, hela zinapotea pasipo kuwa na matumizi sahihi, una madeni sugu yasiyoisha,

SWALI LA KWANZA
 je unatoa fungu la kumi kwa uaminifu?, je wewe ni mwepesi wakumtolea Mungu hata kwa kidogo ulichonacho?, kesi hii haihitaji maombi, inahitaji kubadili mfumo wa maisha yako ya utoaji. Malaki 3:10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi;

mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

 Malaki 3:11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi. Huwa hatumkemei alaye kwa maombi bali kwa kumtolea Mungu halafu yeye Mungu anamkemea alaye.

 Unaweza ukawa mwanamaombi sana lakini huoni mafanikio, si kila kitu kinahitaji maombi kuna vitu vinahitaji kubadili mfumo wa maisha yako. Mwenye masikio na asikie Roho wa Bwana asemavyo. Yupo anaesema mimi siwezi kumtolea Mungu kwasababu nina changamoto nyingi za kiuchumi, pasipokujua changamoto za kiuchumi hutatuliwa kwa kumtolea Mungu ( CHUMA HUNOA CHUMA). Mungu atusaidie.

 Angalia hii, watu wengi wanapoumwa hukimbilia kukemea magonjwa lakini angalia mchakato wa uponyaji unaanzia wapi Zaburi 103:3 Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Kabla hujaomba uponyaji lazima ujichunguze na kuona hakuna uovu wowote ndani yako, na ukigundua kuna uovu na ukautubia na ukaacha uovu wako kabisa hata usipoomba uponyaji, uponyaji utakujilia tu.

 Maana package ya TOBA huja na UPONYAJI. Kama vile mtu unavyonunua kwenye simu yake bando la kuongea lakini anapewa na Mb za internet. Kazi yangu ni kukuombea na kazi yako ni kubadili mfumo wa maisha yako. Kama umenielewa vyema sema Ameen.

 ————————
 Pastor Myamba +255 713 842 123
+255 744 982 517
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

2 comments:

  1. Pastor naomba kujua juu ya hili, Ni nini chanzo cha Israeli kwenda misri kuwa watumwa, pia kwenda babeli kuwa watumwa?

    ReplyDelete