Wengi wa wasomi wa kale wanasema neno Biblia limetoka katika lugha ya Kiingereza BIBLE ambalo pia twafahamishwa kwamba Waingereza nao waametoa katika Lugha ya Wagiriki katika neno BIBLOS ambalo kama lingetafsiriwa moja kwa moja toka Kigiriki kuja Kiswahili basi maana yake ingekuwa ni vitabu.
Biblia kama tunavyofahamu ni moja ya vitabu maarufu na vinavyosomwa na idadi kubwa ya watu tangu enzi na enzi, kumekuwa na aina tofauti ya Biblia kati ya moja na nyingine kwenye idadi ya vitabu vyake kwa mfano kuna Biblia ina vitabu 66 yaani Agano la kale vitabu 39 na Agano jipya 27.
Lakini pia ipo Biblia yenye vitabu 73 ambayo imeongezwa vitabu vijulikanavyo kama “DEUTEROKANONI” ambavyo ni TOBITI, YUDITHI, HEKIMA YA SOLOMONI, SIRA, BARUKU NA 1&2 MAKABAYO.
DEUTEROKANONI
Ni vitabu ambavyo vinapatikana kwenye Agano la Kale la Kigiriki lijulikanalo kwa jina la SEPTUAGINTA.Vitabu hivyo vinakubaliwa na baadhi ya makanisa ya Kikristo kama Wakatoliki kuwa miongoni mwa vitabu vya Agano la Kale, vinaitwa “Deuterokanoni” au “kanuni ya Pili”yaani vilikubaliwa tu vitabu vya Agano la kale na kwa jina hilo vinabainishwa na vile vitabu vingine vya Agano la Kale vilivyo katika Biblia ya Kiebrania “PROTOKANONI” au Kanuni ya kwanza.
Kwa Wakatoliki vitabu hivyo vilitajwa rasmi kuwa vitabu vya Biblia katika Mtaguso wa Trenti mwaka 1546 ingawa makanisa mengine hayathamini vitabu hivyo kuwa vya Biblia.
AGANO LA KALE
Wayahudi wameligawa Agano la Kale katika sehemu kuu tatu ambayo kwa pamoja wanayaita maandiko hayo “TANAKI” neno ambalo limetungwa kwa kutumia herufi za mwanzo za mgawanyo wa vitabu hivyo yaani, TORAH (sharia/torati) NEBIIM (Manabii) KETHUBIM (maandishi) hivyo Biblia ya Kiebrania imegawanyika kama ifuatavyo…
1.TORAH (sharia)
Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu na Torati
2. NEBIIM (Manabii)
Yoshua, Waamuzi,1&2 Samweli,1&2 Wafalme, Isaya, Yeremia ,Ezekiel, Hosea, Yoeli, Amosi, Obadia, Yona, Mika, Nahumu, Habakuki, Sefania, Hagai, Zakaria na Malaki.
KETHUBIM (maandishi)
Zaburi, Ayubu, Methali, Ruthu, Wimbo Bora, Mhubiri, Maombolezo, Esta,Daniel, Ezra, Nehemia,1&2 Nyakati.
Hivyo ndio mgawanyo ulivyokuwa katika Biblia ya Kiebrania na toleo lijukanalo kama “TOLEO LA MASORA”
Itaendelea ..
Na mwandisho wetu
Pascal kapombe
Post A Comment:
0 comments: