Jamii yetu inaamini kuwa wanaofanikiwa wana bahati walipangiwa toka kuzaliwa na wasiofanikiwa nao walipangiwa hivyo hivyo tangu kuzaliwa kitu ambacho siyo sahihi kabisa. Utasikia fulani amepata ile kazi kwa sababu ana bahati. Fulani katajirika kwa sababu ana bahati. 

Kitu wasichokijua watu wa aina hii ni kuwa "BAHATI INATENGENEZWA". Kila mtu amepewa chance ya kuweza kuitengeneza bahati yake mwenyewe. Wewe ndo unaamua kuwa Watu wakuite una bahati au la!! 


Siku moja nilisikia kwenye mahojiano kati ya Floyd Mayweather na Mwandishi wa habari kuwa "Floyd anashinda mapambano kwa sababu ana bahati". Mwingine akasema Bill Gates amefanikiwa sana kwa sababu ana Bahati. Mwingine akasema Watu kama wakina Mark Zuckerburg mmiliki wa facebook ni miongoni mwa watu waliozaliwa na nyota za bahati. Mwingine nikamskia akisema "Kuna mzee alikuwa mchimba madini sasa kapata Tanzanite yenye thamani kubwa wanasema ana bahati sana".

Wataalam wa sayansi ya mafanikio wanatafsiri bahati kwa namna hii ambayo hata mimi niliipenda na kuikubali kwa 100%.Wanasema "LUCK IS WHEN OPPORTUNITY MEETS PREPAREDNESS". Akimaanisha kuwa "BAHATI NI PALE AMBAPO MAANDALIZI YAMEKUTANA NA FURSA".

Kilichomaanishwa hapo ni kuwa Mtu kama Bill Gates kusoma Computer Science na kuwa competent kwenye Programming hiyo tunasema ni PREPARATION(Maandalizi) lakini wakati tayari ana hayo maandalizi ya uwezo mkubwa wa Programming anapata wazo la kuwa na Microsoft Windows ambayo ni FURSA(Opportunity). Kitendo cha mtu kwenda kwenye machimbo hiyo tunasema ni PREPARATION lakini Kupata Tanzanite hiyo ni Fursa. 

Kama ingekuwa bahati basi Microsoft window angetengeneza mtu ambaye hajui hata computer ni nini!!, Lakini bahati hiyo ilienda kwa Bill Gates kwa sababu aliandaa mazingira. Kama ingekuwa bahati Tanzanite hiyo angaipata mtu anayetembea tu barabarani, Lakini aliipata aliye mgodini kwa sababu alikuwa ameshaanda mazingira tayari kwa fursa au bahati hiyo. Mark ametajirika kupitia facebook kwasababu aliandaa mazingira ya kusoma Programming na Psychology.HAWA WATU WOTE WALIZITENGENEZA BAHATI ZAO WENYEWE KWA KUANDAA MAZINGIRA.

HATA WEWE UNAWEZA KUJITENGENEZEA BAHATI YAKO. Simply kabisa Tengeneza kwanza mazingira kisha pambana kutafuta Opportunities (Fursa) then BAHATI YAKO ITAKUJIA.

Mafanikio huwa hayamfuati mtu alipo bali mtu huyafuata mafanikio.  Wenzako wanafungua makampuni mapema baada ya mwaka mmoja wakifanikiwa unasema wanabahati hao walipangiwa na Mungu unasahau kuwa waliandaa mazingira kwa ajili ya bahati zao. Mwenzako ana ndoto kubwa anaanza kidogo wewe umetulia tu akipata fursa kubwa na kutajirika unaanza kusema huyu ni miongoni mwa wale waliopangiwa na Mungu kuwa matajiri unasahau kuwa alitengeneza bahati yake mwenyewe kwa kuandaa mazingira.Mwenzako anajitesa kufanya mazoezi kwa nguvu usiku na mchana wakati wewe umelala na unakula bata halafu akipita kwenye mchujo wa machuano ya vipaji na kujishindia mapesa mengi na kutoboa kwenye kipaji chake unaanza kusea hao ukoo wao wana bahati sana unasahau kuwa alikuwa anakesha kujifua wakati wewe umelala. Mwenzako anapambana kuwa competent (Mbobezi) kwenye professional yake wewe unalala na kumuona anajitesa ikifika kipindi makampuni ya kimataifa yanamng'ang'ania unaanza kusema jamaa ana bahati sana unasahau kuwa amejitengenezea bahati.

"BAHATI INATENGENEZWA GUYS".Ukiwa Muwajibikaji na maisha yako kwa asilimia 100% na kuendelea kupambana kuhusu ndoto yako kila siku bila kulalamika lalamika ndo unajitengenezea bahati yako hivyo.

Live Your Dream!!

Jay Ability

0678798720

Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: