Kuna kusudi la Mungu ndani ya udhaifu wako.
Bwana asifiwe!
Ni siku njema tena ambayo Bwana Yesu ameifanya.Maandiko yanasema ikawa jioni ikawa asubuhi,hata kama kunashida unapitia,asubuhi njema ipo mbele yako.
Ni siku njema tena ambayo Bwana Yesu ameifanya.Maandiko yanasema ikawa jioni ikawa asubuhi,hata kama kunashida unapitia,asubuhi njema ipo mbele yako.
Leo kuna kitu nataka tukizungumzie ambacho naamini kitabadilisha maisha yako na kufikiri kwako. Ili kuelewa zaidi juu ya mada hii tutajikita sana kwenye maisha ya mashujaa wa Mungu kama Daudi na Samsoni. Mada hii itakuwa katika vipengele kwa sababu ni mada ndefu na inahitaji utulivu wa kiroho kuielewa. Jina la Bwana Libarikiwe sana.
1. "SAMSON" MWAMUZI WA MWISHO KWA ISRAEL KAMA KIVURI CHA KRISTO
Samson sio jina geni kwenye masikio ya watu, hata wasiomjua Mungu wengi wanafahamu samsoni ni nani kutokana na Nguvu na uwezo aliokuwa nao ama mwamuzi wa israeli.
Baada ya wanaisrael kumuasi Mungu kwa mara ingine, Mungu akaamua kuwati mikononi mwa wafilisti kwa muda wa miaka 40 (Kuna siri kubwa kwenye namba 40). Baada ya kilio cha Muda mrefu Mungu akawainulia mwamuzi mwingine ambaye hakuwa kama waamuzi wengine kwanzia kuzaliwa mpaka kufa kwake.
Kulikuwa na mzee mmoja ailiyeitwa Manoa pamoja na mke wake ambaye alikuwa amefungwa tumbo asiweze kuzaa.
"Malaika wa BWANA akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume.WAAMUZI. 13:3 "
Mfanano wa kwanza wa samsoni na kristo unaonekana hapa kwenye kuzaliwa kwake. Kipindi Yesu anazaliwa,Malaika Gabrieli alikuja na ujumbe kwa maria na kumbwambia kuwa atamzaa mwana mwanamume ambaye atawaokoa wana wa israeli na Tabu zao. (Mathayo 1:23)
Mungu alimuandaa samsoni kuja kuwa mkombozi kwa waisraeli,mtu ambaye atawatoa waisraeli mikononi mwa wafilisti.Lakini ujumbe huu wa Mungu,kulikuwa na Mambo Mengi yaliyojificha. Tuangalia moja baada ya jingine.
a) "Malaika wa BWANA akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume. kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa MNADHIRI wa Mungu tangu tumboni; NAYE ATAANZA kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.
AMU. 13:3, 5 "
AMU. 13:3, 5 "
-MNADHIRI
Mnadhiri ni mtu ambaye alikuwa anawekwa wakfu kwa ajiri ya kazi fulani ya Mungu ,ni mtu ambaye anatakiwa aishi maisha ya utakatifu maisha yake yote ya unadhiri kwa kufuata taratibu na sheria zote zilizoamriwa.
Mnadhiri ni mtu ambaye alikuwa anawekwa wakfu kwa ajiri ya kazi fulani ya Mungu ,ni mtu ambaye anatakiwa aishi maisha ya utakatifu maisha yake yote ya unadhiri kwa kufuata taratibu na sheria zote zilizoamriwa.
"Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena na watu wa Israeli, uwaambie, Mtu mume au mtu mke atakapoweka nadhiri kubwa, nadhiri ya Mnadhiri, ili ajiweke wakfu kwa BWANA; atajitenga na divai na vileo; hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yo yote ya zabibu, wala asile zabibu, mbichi wala zilizokauka. Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, wembe usimfikilie kichwani mwake; hata hizo siku zitakapotimia, ambazo alijiweka wakfu kwa BWANA, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele za kichwani mwake zikue ziwe ndefu.HES. 6:1-3, 5 "
Kwa hiyo moja kwa moja samsoni aliwekwa wakfu na Mungu mwenyewe kwa ajiri ya kazi ya muhimu sana.
Jambo la Pili alilolieleza malaika na ambalo lina mashiko makubwa ni hili hapa chini
-NAYE ATAANZA KAZI YA KUOKOA WAISRAELI.
Samsoni ataanza kazi ya kuwaokoa waisraeri kutoka mikononi mwa wafilisti,je hii kauli inamaanisha kuna mtu atamaliza kazi? ni nani uyu ambaye atamalizia hii kazi? - Ni Yesu,dhahiri ni Yesu kristo. Hii inaonyesha mfanano mkubwa sana kati ya Samsoni na Kristo (kuzaliwa,kazi zao na hata maisha yao).
Utaweza kuwa unajiuliza mpaka sasahivi kuwa Samsoni anahusika vipi kwenye udhaifu na kusudi la Mungu kama kichwa cha habari kinavyosema? Ondoa shaka,twende pamoja na tutafika na tutalelewana.
Kitu cha mwisho cha mwisho ambacho napenda napenda kukujuza hapa kwenye kuzaliwa kwa Samsoni ni hiki hapa chini.
Manoa akamwambia mkewe, Hakika yetu tutakufa sisi, kwa sababu tumemwona Mungu. Lakini mkewe akamwambia, Kama BWANA angetaka kutuua hangepokea sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, mikononi mwetu, wala hangetuonyesha mambo hayo yote, wala hangetuambia mambo kama hayo wakati huu.
AMU. 13:22-23
Kumbe aliyeleta habari za kuzaliwa kwa Samson ni Yesu kristo mwenyewe. Tumeshasahi kuzungumzia hili katika mada za nyuma kidogo kuwa MIKAEL malaika mkuu ndiye Yesu kristo,na alikuwa anatambulika hivyo kabla ya kudhihirishwa kwenye agano jipya kama kristo.
Katika kipengele kijacho (sehemu ijayo) ,tutazungumzia yafuatayo
1.Yesu na samsoni kazi za Roho na Kazi za Mwili.
2.Samsoni na wanawake wawili.
3. Kristo mwisho wa sheria.
Post A Comment:
0 comments: