Muda mwingi tunapataga shida kwenye maisha (strugless) kwa sababu tumesahau kanuni hii ndogo tu ambayo Bwana Yesu aliitaja kwenye kitabu cha Mathayo
Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
MATHAYO. 6:24
Hapo tutoe neno mali kwa sababu limesimama badala ya shetani. Kwahiyo hiyo sentensi ingesomeka hiviii
Hii ilikuwa unamaanisha,kama hautakubali kuwa pamoja na Yesu,basi wewe moja kwa moja ni wa ibilisi ama shetani,ile dhana ya kuwa mimi sio wa Yesu lakini pia sio wa shetani haipo hapa.Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na Shetani.Sasa hii maana yake nini?hapa mwanzo Mungu alipanda miti miwili tu katika bustani ya Eden.Mti wa ujuzi wa mema na mabaya pamoja na mti wa uzima,hakukuwa na mti mwingi pale bustanini,Only two.
Sasa inawezekanaje kuwatumikia wote? jibu hapa ni HAIWEZEKANI.
Ukimpenda kristo utamchukia shetani,ukimpenda shetani basi moja kwa moja haupo kwa kristo.
Katika dunia ya sasa,watu wengi tunahangaikia sana mali na vitu vinavyofanana na hivyo mpaka inapelekea kutofanya wajibu wetu uliotuleta hapa duniani.
Fedha na dhahabu ni mali ya baba,inamaana ukimfuata baba utapata vyote si ndio? yes
Sasa haiwezekani kutumikia mali na ukampenda Bwana,lazima mali uzitiishe chini ya miguu yako,zisikutawale wewe ndo utawale mali kwa utukufu wa Mungu.Hii ni mbinu ya shetani ya kufanya watu wawe bize sana na Mambo ya utafutaji mpaka wanamsahau Mungu au wanapata Muda mchache sana kwa Mungu na kusahau kuwa Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu na anatamani kuona tunajitoa kwake kuliko sehemu yeyote.
NB: Hii haimaanishi tusifanye kazi ama tusimiliki mali,hasha. Tunatakiwa tumiliki mali zetu pamoja na Yesu.
UTAFUTENI KWANZA UFALME WA MUNGU NA MALI ZINGINE ZOTE MTAZIDISHIWA
Post A Comment:
0 comments: