Je wajua? na kama unajua basi nataka kukujuza zaidi.
Zifuatazo ni baadhi ya sifa za dini pendwa ya kikristo.
 
1. Ukristo ni dini inayosakamwa zaidi ulimwenguni na inaongoza kwa kupingwa na watu wengi. Kiuharisia ni zaidi ya nchi 25 hazitambui ukristo. Nchi kama qatar,Afghanstan,egypt,korea kaskazini na nyinginezo,ni baadhi ya nchi ambazo wakristo wanaishi maisha magumu sana.


2. Kuna makanisa saba bara la ANTACTICA nayo ni

#Chapel of the Snows

#Trinity Chapel

#The Ice Cave Catholic Chapel at Belgrano II Base

#San Francisco de Asis Chapel

#St. Ivan Rilski Chapel, Livingston Island

#Chilian Chapel of Santa Maria Reina de la Paz

#Catholic Chapel of Santisima Virgen de Lujan at Marambio Base

Hii ni hali ya kustaajabisha ukizingatia hali ya bara hili na idadi yake ya watu wanaokadiriwa kuwa 1000 tu.

3. Mnamo mwaka 1969, Chombo cha Apollo - 11 kilitua kwa mara ya kwanza kwenye mwezi kikiwa na watu wa tatu ambao ni

Neil Armstrong, Michael Collins, and Edwin “Buzz” Aldrin

Masaa machache baada ya kufika kwenye mwezi,bwana Buzz anasema alianza kusoma neno la Mungu kutoka kwenye Biblia huku akimshukuru Mjngu kwa nafasi aliyompa. Hii ikapelekea ukristo kuwa wa kwanza kufikiswa nje ya mipaka ya dunia.


Hizi ni baadhi ya sifa kidogo tu za ukristo.Tutazidi kukuletea vitu vingine vizuri zaidi.
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: