UKWELI KUHUSU KUZAMA KWA MELI YA TITANIC (MUNGU HADHIAKIWI),titanic
Mwaka 1912 wakati meli kubwa kuwai kutokea duniani iliyopewa jina la Titanic ikiwa katika safari yake ya kwanza toka kuzinduliwa rasmi mwaka 1911 ikitoka nchini Uingereza na kwenda nchini Marekani ilipata ajali na kuua zaidi ya watu 2,000.


Ni historia ambayo watu wengi wanaitambua tena wengi wakitaja chanzo cha ajali hiyo ni jiwe la barafu lililosababisha kupasuka sehemu ya chini ya meli hiyo na kusababisha maji mengi kuingia na kusababisha kuzama kwa meli hiyo.

Lakini ukitafakari haikuwa rahisi kwa meli kubwa na iliyojengwa kwa ustadi mkubwa kama huo kuzama kwa kupasuliwa kwa na jiwe la barafu.

Urefu wake wa futi 882 na uzito wa tani 52,310 ni jambo gumu sana kuruhusu kupasuliwa kwa jiwe la barafu ambalo lilikuwa baharini na kusababisha kupasuka kwa meli iyo.

Unadhani ni kipi kilikuwa chanzo?
Sababu ni rahisi tu, inapatikana katika kitabu cha Wagalatia 6:7 ambayo inasema
"Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna."

Ilikuwa katika uzinduzi wa meli hiyo ndipo yule muandisi aliyehusika kuijenga meli iyo iliyogharimu paundi milioni 1.5 alipohojiwa na kuulizwa uimara wa meli hiyo na ndipo alisema kwamba uimara wa meli hiyo ata Mungu hawezi kuifanya izame.

Alimdhihaki Mungu na kile alichokipanda ndicho alichokivuna.
Katika safari ya kwanza tu ya meli hiyo ikapata ajali tena sio ilipata ajali kwa manahodha na wafanyakazi kutotambua! waliliona hilo jiwe la barafu lakini wakasema kwa ukubwa wa meli hiyo haitoweza kuangushwa na udogo wa barafu kama hilo.

Mwisho wa siku kikatokea kilichotokea na Neno la Mungu likaendelea kusimama kama alivyosema kwamba "Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele." katika kitabu cha Isaya 40:8
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

1 comments: