UHUSIANI ULIOPO KATI YA MALAIKA MIKAELI NA YESU KRISTO

Kwa watu wengine ,hii dhana ya Yesu kuwa mikaeli ambaye agano la kale linamzungumzia sana kama malaika mkuu,inaonekana kama dhana ambayo haiwezekani kabisa.Na baadhi ya watu wanaona kama hii dhana itakuwa kweli,basi itamfanya Yesu aonekane kama wanadamu wengine na asiwe na utukufu huu wa kiungu ambao anao sasa. 

Pia kuna baadhi ya magroup ya kidini yanatumia mafundisho haya kumtoa Yesu kwenye uungu wake,na kusema Yesu sio sawa na Jehovah Mungu (kitu ambacho sio sahihi).

Kuna mifano mingi kutoka kwenye maneno ya Mungu ambayo inamuonyesha Mikaeli ambaye ndiye malaika mkuu na ndiye mtu wa vita kuwa anaweza kutambulika kama Yesu bila kumtoa Yesu kwenye utatu mtakatifu.
Ngoja tuanze kutazama maandiko kwenye biblia mstari kwa mstari.

1.   KUZALIWA KWA YESU
Yesu alipozaliwa kwenye mwili (tunasema kwenye mwili kwa sababu yesu alikuwako tangu awali) na bikira mariamu katika bethelehemu ya uyahudi,unabii mwingi ulimtambulisha kwa majina tofauti tofauti.

a.    Emanueli (Mungu pamoja nasi) – Mathayo 1:23
b.   Yesu (mwokozi) – Mathayo 1:21
c.    Kondoo wa Mungu – Yohana 1:23
d.   Kristo mesia – yohana 1:41

Haya ni baadhi ya majina ambayo yanamtambulisha Yesu kwenye agano jipya.Tukumbuke pia shetani kabla ya anguko alikuwa na majina tofauti.Kabla ya kuasi shetani alikuwa anaitwa LUCIFER yaani nyota ya asubuhi.Baada ya kuasi,LUCIFER akapata jina linguine ‘SATAN’ au shetani (ISAYA 14:12, UFUNUO 12:9). Sasa kwa sababu tunaamini kuwa yesu alikuwako toka mwazo na kabla hata ya dunia haijakuwako kama YOHANA 1:1 inavyoeleza,inaweza ikaleta maana tukisema kuwa YESU alikuwa na jina lingine kabla ya kuja dunia kama mwokozi. (JINA LA YESU LINATUKIMA DUNIANI KAMA MWOKOZI).

2.   MAANA YA JINA MIKAELI
Katika nyakati za biblia,majina ya watu au vitu yalikuwa na maana kubwa sana.karibia kila jina lilikuwa na maana Fulani.Tuangalie mifano kidogo.
a.    Elijah (Mungu wangu ni muweza)
b.   Danieli (Hukumu ya Mungu).
c.    Gabrieli (Mtu wa Mungu)
d.   Mikaeli (Mmoja anayefanana na Mungu)

Tunafahamu kuwa hakuna kamaMUNGU isipokuwa Mungu  mwenyewe,tukumbuke kilichomshusha shetani ni kiburi cha kutaka kufanana na YESU. Sana kutokana na maana halisi ya mikaeli kuwa mmoja anayefanana na MUNGU,na kuwa lazima yesu alikuwa na jina linguine kabla ya kuzaliwa bethelehemu,ni logic kusema kuwa kuna uwezekana mkubwa Mikaeli ndilo jina alilotumia Yesu kabla ya kuzaliwa na Mariamu.

3.   MIKAELI “ARCH-ANGEL”)
Neno ARCH ni neno la kigiriki lenye maana ya MTAWALA.Kama Mungu alivyomtawala wa kila kitu chenye uhai na kisicho na uhai huku Yeye akiwa sio mwanadamu,Pia Yesu kama ARCHANGEL MIKAEL alikuwa mtawala wa malaika bila yeye kuwa malaika.

Kwahiyo,biblia kumuita Yesu mikaeli the archangel,inamaanisha Yesu ndiye kiongozi mkuu wa malaika wote waliopo mbinguni huku yeye akiwa sio malaika.Hii ni sawa na raisi JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI ambaye ni amri jeshi mkuu huku yeye akiwa sio mwanajeshi,yeye akiwa raisi wa nchi
MWANZO 1:28 Biblia inampa mamlaka mwanadamu juu ya kila kitu ambacho Mungu amekiumba wakiwemo wanyama,wadudu,vitambaaavyo na visivyo tambaa.Kama mwanadamu anaweza kuongoza wanyama huku yeye akiwa sio mnyama,ni Dhahiri kuwa Yesu anaweza kuwa kiongozi wa malaika huku yeey akiwa sio malaika.

4.   AGANO LA KALE NA AMRI JESHI MKUU
Agano lakale lina historia za kusisimua za watu walio wahi kukutana na amri jeshi mkuu.

JOSHUA 5:13-15 “Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yericho,akavua macho yake na kuangalia,na tazama mtu mume akasimama kumkabiri mbele yake,naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake.kawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yericho,akavua macho yake na kuangalia,na tazama mtu mume akasimama kumkabiri mbele yake,naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake.Yoshua akamwende ana kumwambia,je wewe upo upande wetu au upande wa adui zetu.Akasema laah,lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana.Yeshua akapumuka hata nchi,naye akasujudu akauliza,BWANA wangu aniambia nini mimi myumishi wake? Huyo amiri wa jeshi la Bwana akamwambia Yeshua,vua viatu vyako  miguuni mwako,kwa kuwa mahari hapa usimamapo ni patakatifu,Yeshua akafanya hivyo.”

Katika maandiko haya tunaona kuwa Yeshua alikutana na Yesu kama amiri wa Bwana.na hii ilikuwa kawaida kwa Yesu kukutana na watu enzi za agaio la kale katika umbo la kibinadamu.. katika maandiko haya juu,ukisoma kwa biblia ya kiingereza, huyo mtu aliyesimama mbele ya Joshua alijitambulisha kama (I AM COMMANDER IN-CHIEF OF THE LORD ARMY). Kumbe hapa Yesu anaonekana kama amiri jeshi mkuu wa kikosi cha Mungu mbinguni,lakini maandiko hapo juu yapo wazi kabisa kuwa huyo mtu akuwa malaika wa kawaida kwa sababu zifuatazo.

a.    Joshua alianguka na kusujudu.Kama huyu angekuwa malaika wa kawaida,basi angemkataza kumsujudu kama malaika walivowakataza watu walioanguka na kuwasujudu kwenye maandiko kwa kuwaambia kuwa wao walikuwa watumishi tu (UFUNUO 19:10 na UFUNUO 22:8-9). Katika maandiko haya,yohana ana katazwa kumwabudu malaika na kumwambia mwabudu Mung utu.

b.   Huyu mtu mtakatifu alipokutana na Joshua,sio tu alikubali kuabudiwa,ila pia alimwambia Joshua avue viatu kwa sababu mahali pale ni patakatifu.Hii nisawa na kipindi cha Musa alipotokewa na Mungu katika kijiti kilichowaka moto bila kutoketea na sauti ikisikika ikisema VUA VIATU MAHALI HAPA NI PATAKATIFU.Hii ni Dhahiri yule mtu aliyekutana na Yeshua alikuwa ni mwanadamu Yesu kristo.Hapa ndipo maandiko yameweka wazi kuwa kiongozi wa malaika sio malaika wa kawaida bali ni Mungu mwenyewe.

5.   MIKAELI KAMA PRINCE
Kuna baadhi ya maandiko yana mtafsiri mikaeli kama kama mtu spesho,mtu ambaye sio wa kawaida.Mano mzuri wa hili upo kwenye  DANIELI 8:16 NA 9:21.Katika maandiko hapo juu,malaika GABRIEL anamwambia DANIELi kuwa mikaeli kuwa ni mtu maalumu sana mbinguni na kuwa ndiye anayewaangalia watu wake. Prince ni mtoto wa mfalme na Yesu ni mtoto wa Mungu baba.DANIELI 9:25 DANIELI anamuite MESSIAH “PRINCE”

6.   UTATA WA YUDA 1:9
“Lakini mikaeli mkuu aliposhindana na ibilisi na kuhojiana naye kwa ajiri ya mwili wa musa,hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu,bali alisema BWANA NA AKUKEMEE”
Huu ni mstari pekee unaotumiwa na watu ambao hawaamini kuwa mikaeli ni yesu,kwa sababu mikaeli anaonekana kumkemea shetani kwa jina la Bwana.Watu wanasema kuwa mikaeli the archangel hawezi kuwa Bwana kwa sababu yeye mwenyewe anamuita mtu mwingine Bwana. Sasa kwa changamoto kama hii,ni vizuri kuacha Biblia ijichanganue yenyewe.

YUDA 1:9 Inafanana na ZAKARIA 3:2 inayosema “Bwana akamwambia shetani,na Bwana akukemee” tofauti ya mistari hii miwili ni majina tu,sehemu moja ni mikaeli na sehemu ingine ni yesu.Mtu mwingine anaweza sema kuwa katika mistari hii miwili ,Yesu/mikaeli anamuita Baba yake wa mbinguni amkemee shetani.

Au kwamaana ingine unaweza ukasema Yesu alikuwa anajisema  kwa nafsi ya tatu mwenyewe katika YUDA 1:9.Hii nisawa na ule mstari wa agano jipya Yesu aliposema “JE,MWANA WA ADAMU ATAKAPOKUJA ATAIKUTA IMANI” hapa alikuwa anajisema yeye mwenyewe kwenye nafsi ya tatu. kwa wale waliosoma Kiswahili wataelewa Zaidi hapa.

KWA MAELEZO HAYA UNAWEZA UKAPATA UKWELI KUWA KUNA UWEZEKANO WA ASILIMIA NYINGI SANA,YESU KUWA NDIYE MIKAELI.

YESU KUWA MIKAELI HAKUUPUNGUZI UUNGU WAKE,BALI NI JINA TU AMBALO ALILITUMIA KIPINDI CHA AGANO LA KALE.

HATA KAMA HAUAMINI KAMA YESU NDIYE MIKAELI, HAIPUNGUZI UAMINI WAKO KWA YESU.

KUNA MUDA MAANDIKO YANAFICHWA SANA, LAKINI MUNGU ANATUAGIZA KUCHUNGUZA VITU.
MAANDIKO YANASEMA,NI UTUKUFU WA MUNGU KUFICHA JAMBO,BALI WA MFALME KUCHUNGUZA JAMBO – MITHALI 5 : 2


Mungu akubariki sana.
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

1 comments:

  1. je HII WANAYO ITA
    (HOLLY TARISMAN OF SAINT MICHAEL)
    Ni Nini????

    ReplyDelete