Mtu wa kwanza Mungu kumuumba duniani alikuwa ni mwanaume. Mungu alimuumba mwanamme kwa mfano wake na kwa sura yake ili atawale na kuitiisha nchi kama mfalme. (Mwanzo 1:26). Mwanzo 2:7 “BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai (NDIYE ADAMU WA KWANZA).- Mke mwema, mme mwema, sifa za me mwema, mme wa kwenye biblia,


Mtu wa kwanza Mungu kumuumba duniani alikuwa ni mwanaume. Mungu alimuumba mwanamme kwa mfano wake na kwa sura yake ili atawale na kuitiisha nchi kama mfalme. (Mwanzo 1:26).                        

  Mwanzo 2:7 “BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai (NDIYE ADAMU WA KWANZA).

Baada ya hayo ndipo Mungu akamfanya mwanamke,tuwe makini hapa… AKAMFANYA MWANAMKE KUTOKA UBAVU WA ADAMU. Kumbe mwanamke hakutengenezwa kwa mavumbi kama adamu, bali alifanywa kutoka sehemu ya adamu . (MWANAMKE NI SEHEMU YA MWANAUME) (MWANAMME SIO SEHEMU YA MWANAMKE). Kumbe lengo la Mungu kufanya hivyo lilikuwa ni kumpa mamlaka na majukumu adamu ya kuhakikisha anaitunza iyo sehemu yake kama Bwana Mungu anavyotaka. MWANZO 2:21

Kuna kitabu kinakuja kinaitwa “A LOVE STORY – A BOOK OF KNOWLEDGE FOR MAN AND WOMEN” Ndani kinaelezea vizuri sana juu ya huyu mwanamke ambaye Adamu alikabidhiwa na Mungu mwenyewe jinsi alivyokuwa rafiki na mke kwa adamu na kupelekea kutimiza agizo la Mungu la kuwa mwanamke atakuwa msaidizi wa mwanamme.

Kwa maana hii, lazima tuwe na uhakika kwamba, Mungu tayari alikuwa ameshamuandaa mwanamme ama Adamu kuwa na mke. Alikuwa tayari ameshaweka sifa za mume ndani yake, ambazo zitamfanya Adamu amuwezeshe mwanamke wake kutimiza wajibu wa Mungu.

ZIFUATAZO NDIZO SIFA ZA MWANAMME AMBAYE MUNGU AMEMKUSUDIA KUWA NA MKE.

1. KUABUDU (THE ART OF WORSHIPING)
Kitu cha kwanza Mungu alichokifanya kwa Adamu baada tu ya kumuumba ni kumuweka katika bustani ya mashariki mwa Eden kwenye uwepo wake. Maandiko yanasema kuwa ilikuwa kawaida ya Mungu kushuka na kuongea na Adamu uso kwa uso (kwa sababu alikuwa Edeni kwenye uwepo wa Mungu).4

BWANA Mungu alitambua mapema kabisa kuwa , ili huyu mtu ambaye atakuja kuwa kichwa kwa mkewe ,ili aweze kuyatenda mapenzi yangu na kutimiza kusudi la kuwa Mume,Lazima kwanza awe kwenye uwepo wangu,awe mtu wa rohoni,awe mcha Mungu na asitoke Edeni yaani penye uwepo wangu. Adamu alikaa uweponi mwa Mungu siku zote ,akifanya kazi alizokuwa ameagizwa na baba yake mpaka hapo Mungu alipoona ni muda sahihi kwa Adamu kuwa na Mke.

Ni ajabu sana kuona kadri miaka inavyozidi kwenda,vijana wakiume wanazidi kuoa nje ya mpango wa Mungu,nje ya makusudi ya Mungu, wanaume wanaoa nje ya uwepo wa Mungu kama Mungu alivyokusudia. Wanaume ambao Mungu amewakusudia kuwa wafalme na vichwa kwa wake zao,cha ajabu hawamjui Mungu kabisa na wala hawamtafuti. Hii ndiyo chanzo kikubwa cha mafarakano kwenye mahusiano na kwenye ndoa, kwasababu mwanamume umeacha njia Mungu aliyoiweka na kufuata njia zako mwenyewe.

Mwanamme, kaa katika uwepo wa Mungu, Muombe Mungu naye ndiye atakayechukua ubavu wako na kumfanya Eva wako ambaye atakuwa chanzo cha kutimiza makusudi ya Mungu kwenye maisha yako.

Mwanamke, kitu cha kwanza ambacho unatakiwa ukifahamu kwa mwanaume anayetaka kukuoa, ni UHUSIANO WAKE NA MUNGU na sio kama anakupenda au kama ana mali au fedha. Kama mwanaume anamahusiano mazuri na Mungu basi uwe na uhakika kuwa amekuja sehemu salama.

ZABURI 37: 23 “HATUA ZA MWENYE HAKI HUONGOZWA NA MUNGU”

Mungu ndiye awe dereva wa maisha yako ukiwa uweponi mwake. Mungu awabariki sana..Tukutane kwenye sehemu ya pili ambapo tutaangalia sifa zingine 4 za mwanamme mfano wa Adamu ambaye Mungu amemkusudia kuwa mume kwa mkewe.

Itaendeleaa…………………………

Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: