Kwanini na kwasababu gani Mungu alitaka kumua musa? haya ni maswali mawili ambayo watu wengi wanajiuliza wakisoma KUTOKA 4:24-26.
Baada ya Musa kupewa maelekezo na Mungu ya namna ya kuwatoa wana wa israeli katika nchi ya misri,akaanza safari yake kutoka nchi ya midiani  kuelekea misri akiwa na mkewe aliyeitwa sipora na mtoto wake gershomu.
Wakiwa njiani kuelekea sehemu yakupumzikia,biblia inatuambia kuwa Mungu akataka kumuua musa.Hapa ndipo kwenye utata kwa watu wengi.
1.Kwanini Mungu atake kumuua musa wakati ndiye aliyemtuma na kumchagua kuwatoa waisraeli katika utumwa misri?
Sababu zipi zilifanya Mungu atake kumuua musa?
Tuangalie kwanza hayo maandiko ndipo tuyachambue.
KUTOKA 4:24-26
"ilikuwa walipokuwa njiani mahali pakulala,BWANA akakutana naye akataka kumuua. 25, Ndipo sipora akashika jiwe gumu,na kuikata govi ya zunga la mwanawe na kuibwaga miguuni pake,akasema,hakika wewe u bwana harusi wa damu kwangu mimi 26; Basi akamuacha,ndipo huyo mkewe akanena..."
Biblia haizungumzi ni namna gani Mungu alikutana na Musa.Kama ni ana kwa ana au kwa aina nyingine yeyote. Lakini kitendo cha Mungu kutaka kumuua Musa ukisoma hayo maandiko utagundua kuwa kilikuwa cha taratibu.Mungu amewapa adhabu kama hizi za kifo watu wengi kwenye biblia akiwemo anania na safira  ambao walikufa ghafla kwa kuasi,pia na wana wa kola ambao ardhi iliwameza baada ya kuasi.
Sasa kuhusu musa,maandiko hayaonyeshi Mungu alitaka kumuua kwa namna gani,ila tu kwa sababu sipora ambaye ni mke wa musa alipata muda wa kukata govi la mtoto wake (kumtahiri mtoto wake) maana yake Mungu alifanya kifo cha musa kisiwe cha ghafla kama anania kwasababu bado alikuwa na mpango na musa,mfano HOMA KALI.
Musa alifanya dhambi na ndio maana Mungu alitaka kumuadhibu.watu wengi wanakuwaga na maswali mengi juu ya dhambi alioifanya musa,na wengine husema huenda dhambi yake ilikuwa ni kumuua yule mtu misri,hasha,dhambi aliofanya musa ni kutomtahiri mtoto wake kama Mungu alivyogiza enzi za ibrahimu kutahiriwa kwa kila mtu atokae kwenye viuno vya ibrahimu,na musa ni chimbuko la ibrahimu.Kushindwa kumtahiri mtoto wake,maana yake ni kwenda kinyume na agano la Mungu alilolofanya na Ibrahimu miaka Mingi iliyopita akimuagiza kumtahiri kila mtoto wa kiume kama alama na ishara ya agano lake.
(MWANZO 17:9-14).
maandiko yanasema wazi kabisa juu ya watu wasiotahiriwa sawasawa na agano la ibrahimu kuwa watakufa
na roho zao zitatengwa.Musa asingeweza kwenda kufanya kazi ya Mungu na kuwafundisha watu taratibu za Mungu kama yeye mwenyewe ni muasi na hamtii Mungu,Mungu ilibidi amfosi kumtahiri mwanae kwa kutaka kumuua yeye mwenyewe.Baada ya mkewe kumtahiri mtoto na kuweka damu kama ishara ya upatanisho juu ya miguu ya musa,Mungu akamuacha musa na kifo kikaondolewa kwake.
UTII... Ndiyo kosa la musa kubwa ambalo lilitaka kummaliza musa. Yatupasa kuwa watii,hata kama ni watumishi na tunatembea na Mungu,kama musa alivyotakwa kupigwa na Mungu,vile vile nasi Mungu anaweza akatupiga kwa kukosa kutii.
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

2 comments:

  1. Asante kwa maelezo mazuri, ubarikiwe.

    ReplyDelete
  2. Hakika nimeelewa nini chanzo cha Mungu kutaka kumuuwa musa

    ReplyDelete