Huu ni mwendelezo wa sehemu ya kwanza ya maana halisi na jinsi ya kuingia ulimwengu wa roho.
Ayubu 8:9
Maandiko haya yanaonesha ni jinsi gani maisha yetu ni kivuli.Hii inamaanisha kuwa kama kuna kivuli(maisha yetu),basi kuna kitu ambacho kinatoa kivuli hicho ambacho ni roho zetu.
Maandiko haya yanaonesha ni jinsi gani maisha yetu ni kivuli.Hii inamaanisha kuwa kama kuna kivuli(maisha yetu),basi kuna kitu ambacho kinatoa kivuli hicho ambacho ni roho zetu.
Mungu alikuwa na mpango wa wanadamu waishi rohoni tangu alipoweka misingi ya dunia-
Mwanzo 1:3
Mwanzo 1:3
Nuru ambayo Mungu anaizungumzia kwenye haya maandiko ni Nuru ya rohoni ambayo aliiumba mara tu baada ya kuumba ulimwengu,Nuru hiyo ya rohoni ilidumu mpaka Mungu alipoumba Nuru ya mwilini(jua na mwezi) ambacho iikuwa ni kivuli cha Nuru ile ya mwanzo.
Adamu alikiwa mtu wa rohoni tangu Mungu alipomuumba na ndio maana alikuwa nauwezo wa kuongea na Mungu uso kwa uso,angekuwa mwilini asingeweza kuongea na Mungu.Maandiko yanasema "Mungu ni roho,na wamwabuduo(wamwendeao) yawapasa kuwa katika roho"
Hapa kote tunajaribu kuangalia Maana halisi ya ulimwengu wa Roho.Ulimwengu wa roho ni halisi kabisa ila cha ajabu wanadamu wengi hasa tunaoamini neno hatuutambui na hatuna mpango nao..
Mwanadamu amegawanyika kwenye sehemu kuu tatu.
1.Mwili
2.Nafsi(akili) kwa ajiri ya kufikiri na
3.Roho.
-1thesalonike 5:23
1.Mwili
2.Nafsi(akili) kwa ajiri ya kufikiri na
3.Roho.
-1thesalonike 5:23
ila cha ajabu ni pale ambapo watu wa Mungu anatumia miili na akili zao vizuri sana ila hawana mpango na Roho angali hakuna kitu ambacho kinawezekana kufanyika au kutokea mwilini bila kupitia rohoni.
Wachawi na waganga wanawaonea wakristo wengi kwa sababu ya uwezo wao wa kwenda kwenye ulimwengu wao wa roho vizuri na kuuathiri ilibulete mabadiliko.Wanatumia Damu,na maombi ya aina yao ikiwemo mifungo yao ili wafanye mabadiliko kwenye ulimwengu wa roho na kuleta mateso kwetu.
Lakini ashukuliwe yesu kristo ambaye Ametuketisha juu sana mbali na falme na mamlaka za shetani.
Ulimwengu wa Roho ambao yesu kristo ametupa una nguvu sana kuliko wa shetani.-Luka 10:19
Mamlaka ambayo yesu anayazungumzia hapa yapo kwenye ulimwengu wa roho na Maandiko yanasema "Hakuna kitakacho tudhuru"-hii inaonesha authority au mamlaka juu ya shetani lakini kama tutajua jinsi ya kuutumia ulimwengu wa roho.

Kufanikiwa kwetu,Nguvu zetu,afya zetu,elimu zetu na mafanikio yote yapo kwenye ulimwengu wa roho na bila kuujua vizuri basi kila siku tutakuwa watu wa kulia na kulalamika.
WAEFESO 1:3
Mungu ametubariki kwa baraka za aina zote,lakini ameziweka rohoni ambapo alikusudia tuwepo tangu awali.
Mwl.Mtebe anafananisha baraka hizi kama fedha ambazo zipo benki.kama hujui jinsi ya kwenda benki na kutoa pesa izo ili uzitumia,basi utaweza kufa masikini wakati pesa zipo benki.

Wakristo wengi wanakufa au wanaishi kwa shida angali fedha zao zipo benki,watu wanatembea na hundi za utajiri,hundi za afya,hundi za elimu lakini hawajui jinsi ya kuzitumia.
Kumbe kuzipata hizi pesa ni lazima uende benki na ujue jinsi ya kuzitoa.vile vile lazima tujue namna ya kwenda kwenye Roho na kuuathiri huo ulimwengu ili tuweze kupata baraka zetu.
Sehemu ijayo tutaangalia namna ya kuingia kwenye ulimwengu wa roho ili uweze kuuathiri ipasavyo na jinsi ya kukabiliana na changamoto za huo ulimwengu mpya ambao ni wazamani.
Itaendelea...
Barikiwa sana mtumishi
ReplyDeleteI like
ReplyDelete