KATIKA MAMBO HAYO YOTE AYUBU HAKUFANYA DHAMBI.
AYUBU 1:20-22
AYUBU 1:20-22
20 Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia;
21 akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe.
22 Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu.
21 akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe.
22 Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu.
Baba Ninakushukuru kwaajili ya siku ya leo, nakutukuza nakuinua ninakusifu kwamaana unastahili heshima utukufu sifa tukuzo peke yako, asante kwaajili ya asubuhi hii ambayo umetupa kulitafakari Neno lako, Baba ninafungua kila masikio ya rohon ya mtoto wako anaesoma ujumbe huu, mpe vitu vya kujifunza katika Neno lako na ukampe kuvifanyia kazi, katika jina la Yesu Kristo nimeomba na imekua AMENI.
Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu, tukisoma habari za Mtumishi wa Mungu Ayubu tunapata vitu vingi sana vyakujifunza, na Ayubu alikua mwanadamu kama sisi alipita majaribu makubwa, alipita mapito makubwa, kwa kizazi chaleo ingekua mtu anapitia majaribu kama yale angeweza kumuacha Mungu, angetoa maneno yakufuru na mazito juu ya Mungu, angebaki analia kuwa Mungu amemuacha na wokovu angeuacha, lakini Ayubu hakuwaza kumkuru wala kumtenda Mungu dhambi bali alirudi kwenye Neno haraka akasema nalikuja uchi nitaondoka nii uchi, nilikuja sina kitu nitaondoka sina kitu
Ukiyatazama hayo maneno unaweza kusema ni madogo, unaweza kusema ni yakawaida sana lakini ni mazito sana, nafsi yake iliumia lakini akakumbuka alikotoka, aliumbwa akiwa hana mali, wala watoto lakini Mungu alimbariki na akampa kila kitu cha thaman katika dunia hii, akampa utajiri mkubwa sana, alipokumbuka alipotoka akasujudu, maana yake akamtukuza Mungu, akampa heshima Mungu ambae ndie mtoaji na ndie mtwaaji wa vyote.
Mwana wa Mungu unapitia katika majaribu gani, unapitia changamoto gani, je umekosa Ada, je umekosa hela ya pango, je umekosa hela ya chakula, je umeishi maisha ya taabu na kukataliwa, unakili nini mbele za Mungu, unakili nini mbele za wanadamu, unakiri nini ukiwa sirini, mawazo yako yanakiri nini, mwana wa Mungu unakiri nini??? majaribu na changamoto za maisha sio mwisho wa dunia, majaribu na changamoto sio ndio mwisho wakumuacha Mungu na kuhangaikia maisha yako wewe mwenyewe bali nikuzidi kumtukuza Mungu na kutamka na kukiri mbele za watu kuwa punde tu nitapita katika hali hii na kupokea baraka zangu.
Haijarishi unapitia kitu gani wewe mtukuze Mungu, mrudishie Mungu utukufu maana yeye ndie anaestahili sifa shukran wakati wote, Biblia inasema baada ya majaribu yale Ayoub alikuja kubarikiwa zaidi ya mara ya kwanza.
Weka mkazo kwenye Neno, weka mkazo kwenye maombi utapata kufahamu nini chakufanya, ili uvuke katika hayo majaribu, unaposoma Neno utakutana na mahali uombe vipi, maana si majaribu yote ni ya Mungu bali mengine ni utaabishaji wa shetan ili umuache Mungu, hivyo yakupasa upambane kiroho kwa maombi ili utoke hapo ulipowekwa, utoke ulipofungwa, semesha mbingu, semesha ardhi, semesha bahari kote walipo kuweka wakutapike, kila baraka zako zilipozuiwa ziachiliwe kwa damu na jina la Yesu, maombi hayo sio ya dakika tano au kumi, ni maombi ya masaa, maombi ya muda Mrefu, kwanini uombe muda mrefu kwasababu chukulia mfano unapofua kadiri unapozidi kuifua nguo iliyochafu ndipo uchafu unapoiachia nguo na nguo kutakataka ndivyo katika maombi inavyokua kadili unavyoomba sana vifungo vinakuachia, naamini kwamfano huo umenielewa, omba muda mrefu, omba nyakati zote, omba asubuhi, omba mchana, omba jioni, omba usiku, wekeza kwenye maombi omba mpaka upokee jibu lako, omba mpaka milango ifunguliwe kwani mathayo inasema bisheni nanyi mtafunguliwa, hivyo bisha kweli katika maombi utapokea haja ya moyo wako.
Ukiwa hujui jaribu ni la nani omba ikiwa ni mpango wa adui kuniangusha kuniharibu vunja, halibu sambalatisha mipango yake yote, na ikiwa ni mipango ya Mungu mwambie Mungu akupe uvumilivu wa kupita kwenye hayo majaribu na kuvuka salama, usiombe akutoe kwani akikutoa kabla hujaiva kwenye hilo jaribu utapokea baraka kidogo ila ukiiva utapokea baraka stahiki na jaribu lako, kama kuchukiwa acha watu wakuchukie sana, kama njaa acha iume kweli tambua na weka akilini Mungu yupo nawe na baada ya kupita hapo utabarikiwa sana.
Usiache kuomba, omba kwa bidii, kila siku omba, na ukiona siku unaanza kuona uvivu wa kuomba anza na maombi ya vita, piga anga, piga bahari piga nchi, Tumia Isaya 41:11-15, omba mstari mmoja baada ya mmoja utaona unapata chachu ya kuomba zaid, shetan huwa anakawaida ya kufifisha maombi anakutia uvivu wa kuomba, anapoona umegusa mahali pa wewe kutoka ambapo umeshikiliwa ndipo anakutia uvivu usiombe ndio maana nakwambia unapoona husikii hamu ya kuomba wewe omba, ukisikia uvivu wakati wa kuomba force kuomba, pambana katika maombi mpaka utoke ulipowekwa.
Nakutakia baraka za Bwana, acha kulalamika, acha kuongea yasiyo mpendeza Mungu kwani unapanda kupitia hayo maneno ya kinywa chako itafika hatua utavuna hivyo unavyovitamka na kuviwaza moyoni, waza yanayo mpendeza Mungu, tamka ukuu wa Mungu kupitia hiyo adui anashindwa juu yako.
Mungu akubariki sana.
Post A Comment:
0 comments: