Shaloom wapendwa katika bwana,ni siku nyingine njema ambayo tunakila sababu ya kumshukuru na kumtukuza bwana yesu kwa upendo wake usio na upeo wa kutuwezesha sisi kuiona siku ya leo tukiwa na afya ama la ni wagonjwa lakini bado mungu anatuwazia mema siku zote.
Maandiko yanasema katika
Yeremia 29:11 - Mungu anayajua mawazo anayotuwazia,ni mawazo mema siku zote na wala sio mabaya.
Wapo watu wengine wanasemaga kuwa mungu anatupatiaga mambo mabaya mara nyingine,hasha si kwelii kama utasoma kwa makini yeremia 29 utagundua haya,mungu wetu anatuwazia mema siku zote.
Farijika na maandiko haya
"Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo" Yesu;
FLP. 1:6
Hapo tunaona vitu viwili "Yeye aliyeanza kazi njema" Ni nani uyu?
Bila shaka huyu ni yesu kristo aliyeutoa uhai wake kwa ajiri ya ondoleo la dhambi ili kila amwaminiye awe na uzima wa milele na asipotee katika ile mauti ya pili yaani moto na kiberiti.
Baada ya adamu baba yetu kufanya dhambi katika edeni,Binadamu wote tulihesabiwa wafu mbele za mungu,Mungu alijitahidi kumrudisha binadamu katika edeni au uzima wa milele kwa kutumia manabii kama wakina musa,yoshua nk,lakini ilishindikana.
Ndipo biblia inasema mbingu ikawa kimya,wazee ishirini na wanne wakawa kimya,kila mtu mbinguni akanyamaza wakati mungu akiuliza nimtume nani akamwokoe mwanadamu.
Ndipo yesu akasema nitume mimi nikawaoke wanadamu na dhambi zao.
Yeye aliyeanzisha wokovu wako ndiye huyo atakaemaliza kazi yake,usife moyo mpendwa bwana bado anakupenda sana.
Je,upo tayari kumkabidhi yesu maisha yako? unamchango gani kwenye hili.Tunaomba maoni yako
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: