💥BIBLE STUDY💥
Program: Christian theology & systemic theology.
(Kijana Mkristo-KM)

Utangulizi
----------------

🕸️Bwana Yesu asifiwe. Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu kwa wakati huu ambao ametupatia sisi watoto wake ili tuweze kujifunza kutoka kwake. Nina amini kabisa ya kwamba elimu hii utakayoipata itakusaidia kukua kiroho. Kama vile Mimi Mungu alivyonisaidia kupata Elimu hii,na mimi naileta kwenu. AMEN

🕸️Christian Theology.
--------------------###----------------------

Tunavyoanza hii kozi, ni vizuri kuianza kwa kujua kwanza maana ya baadhi ya maneno ambayo tutakuwa tunayaangalia kwa muda mrefu kwenye hii kozi.

kijana mkristo(tzworships)


1. "Theology"
Hili ndilo neno la kwanza ambalo tunaanza kuliangalia. Tunamaanisha nini tunaposema "Theology"

THEOLOGY ni sayansi ya Mungi. Ndio sayansi ya Mungu. Wala usishangae kwa sababu inaitwa sayansi ya Mungu. Au unaweza kuita somo la Mungu au study of God.

Neno "Theology" limetokana na muunganiko wa maneno mawili ya kigiriki.
"Theos" - likimaanisha Mungu na "Logos" likimaanisha somo au study of. Kwa hiyo neno THEOLOGY maana yake halisi ni somo la Mungu au somo la kumjua Mungu au nisomo la kumfikiria Mungu..thinking of God.

🕸️Ni muhimu kutambua kuwa, kwa sisi wanadamu hakuna kazi kubwa na ya muhimu ambayo tunaweza kuifanya tukiwa hapa duniani zaidi ya kumsoma na kumjua Mungu.

Yesu mwenyewe alisema haya. Mtu tu anapomuamini Yesu,hapo hapo anaanza kumjua Mungu. "Anaanza" maana yake zipo hatua nyingine za kufuata ili kumjua Mungu zaidi.

"Mjue sana mwana wa Adamu ili uwe na amani" - Yesu

"Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
YN. 17:3 " - SUV

Maisha ya MKRISTO ni mahusiano au fellowship kati ya muamini na Muumbaji wake. Mahusiano haya yanakuwa zaidi na kukomaa pale muamini anapojifunza na kutaka kumjua sana Mungu au muumbaji wake.

🕸️Paulo mtume alizingumza kitu kimoja cha msingi sana ambacho kimsingi ndio msingi wa muamini. Njia pekee ya kukua kiroho na kuwa tajiri wa ulimwengu wa Roho ni kwa kumjua Mungu sanaaa.

"kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote;"
1 KOR. 1:5
------###-------

🕸️VITU VYA MSINGI KUVIJUA JUU YA SOMO LA MUNGU "THEOLOGY"


1. Kila mtu ana imani yake juu ya Mungu.

Watu wanaosoma theology kama profession au kada wanaitwa theologians. Lakini kimsingi kila mtu ni mwana theologia. Hii ni kwa sababu kila mtu ana kitu anakifahamu juu ya Mungu. Hiyo elimu tu uliyonayo juu ya Mungu inatosha kabisa kuwa Theologian na wewe. Hii ni hata kwa wale ATHEISTS au wapagani ambao hawamjui Mungu. Haya ni mambo ya msingi ambayo inabidi uyajue kwa sababu tutayatumia sana uko mbeleni.

2. Imani uliyonayo ndiyo inayo athiri maisha yako (your belief affects your life).

🕸️Haya mawazo ambayo tumeyaona hapo juu juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa Mungu au vile unavyofikiri juu ya Mungu ndiyo yanayo athiri maisha yako.

Kwa mfano: yule mwenye imani juu ya kuwepo kwa Mungu na ya kwamba tunaweza kumfahamu Mungu,basi tutafanya mambo yatakayo mfurahisha Mungu. Na kama tutakataa idea au wazo la uwepo wa Mungu, basi tutaishi maisha tunayotaka sisi bila hofu wala wazo la kuwa kuna siku itabidi tusimame mbele ya huyu Muumbaji na kijieleza

Paulo mtume aliongea maneno haya kwa mifano akimuelezea timotheo aliyekuwa mwanafunzi wake.

🕸️Mtu awaye yote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa, amejivuna; wala hafahamu neno lo lote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya;
1 TIM. 6:3‭-‬4

🕸️Hapo ndipo ulipo msingi wa imani yetu,kwenye kumjua Mungu.

Huo mstari tuliouona hapo juu, tutakuja kuona maana yake kadri tunavyozidi kusoma kwenye kozi hii.

3. Christian theology ni somo la Mungu wa kwenye biblia. Ukumbuke nimekwambia kwamba theology ni somo la Mungu, na Mungu wapo wengi. Infact hata shetani ni Mungu.

🕸️Mungu sio jina, Mungu ni cheo tu. Mungu wetu haitwi Mungu, anamajina Mengi tu (mfano: Yahweh). Kwahiyo, Christian theology ni somo la Mungu wa kwenye biblia na si Mungu mwingine.

4. Katika Theology, tunasima facts ambazo tayari zipo. Kazi yetu ni kuprove hizo facts.

5. Chanzo cha THEOLOGY ni biblia.

6. MUNGU ametufunulia haya mambo kwa sababu sisi ni rafiki zake. Pale tu unapomwamini Yesu,unakuwa rafiki yake.

Usiku mmoja kabla ya kusalitiwa aliongea maneno haya.

"Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu."
YN. 15:15

Cha mwisho siku ya Leo.
Ukweli huu ambao Mungu ameufunua kwetu hauwezi kueleweka kwa Mtu ambaye hamuanini yesu.


🕸️ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu. Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika; bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;
1 KOR. 2:5‭-‬8

🕸️Kipindi kijacho tunaanza kuangalia HISTORIA YA KANISA NA MUNGU ALIUNGANISHAJE KANISA LA KALE.

Mungu awabariki sana

By
Maestro

YouTube: kijana mkristo
Instagram: kijana_mkristo
Web : Tzworships.blogspot.com
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: