ANZA SIKU NA BWANA
KWA NENO NA MAOMBI
NENO LA MUNGU LINA NGUVU KULIKO NENO LA MWANADAMU
MATENDO 1:8
8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Mpendwa jifunze;
■ Kupokea nguvu za Roho Mtakatifu.
■ Kuwashuhudia wengine habari za Yesu.
Mpendwa,
1.Je, wewe umejazwa
Roho Mtakatifu?
2.Je, wewe una nguvu
za Roho Mtakatifu?
3.Je, wewe unafahamu
utendaji wa Roho
Mtakatifu?
TAFAKARI
Mpendwa, watu wengine hawafahamu umuhimu wa Roho Mtakatifu ndani ya mkristo.
👉🏽Hapa tutadondoa kidogo tu,
KAZI ZA ROHO MTAKATIFU NDANI YETU.
1.Hutuombea kwa Mungu Baba maana ndiye anayeujua moyo na mapenzi ya Mungu.
Warumi8:26
2.Hutufanya tumtambue na kumtukuza MUNGU.
Yohana 16:14
3:Anatuongoza katika kweli yote.
Yohana 16:13.
4:Anatupa uwezo na ujasiri wa kuwaambia wengine habari za BWANA YESU.
Yohana 15:26,
5: Anatufundisha. Yeye ni mwalimu wa kila jambo/ kitu.
Yohana 14:26.
6:Hupanda na kutoa matunda ya Roho ndani yetu.
Wagalatia 5:18-23.
Roho Mtakatifu ni MSAIDIZI WETU.
Barikiwa sana mtu wa Mungu. Uwe na Jumapili njema sana.
Post A Comment:
0 comments: