Kumbukumbu la Torati 4:
✍🏾 Katika hotuba hii tunazidi kuona mzigo aliokuwa nao Musa wa kuona kuwa wana wa Israeli wanakuwa waaminufu kwa Mungu ili Bwana Mungu akawape baraka zake.
✍🏾 Lakini kabla hatujafika mbali, tunaona fungu la kwanza Musa akisema, _”Ee Israeli sikilizeni amri na hukumu niwafundishazo, ili mzitende …”_
✍🏾 Mwonekano wa kuwa Musa aliongea na Israeli ‘yote’, utakuwa unamaanisha kundi la viongozi wanaowakilisha Waisraeli. La sivyo, hakuna namna angeweza kuongea na kundi la watu takribani milioni 2 kwa pamoja bila kuhitaji miundombinu ya kisasa. Kukupa taswira, idadi ya watu milioni 2 ni idadi ya watu wa nchi ya Gabon (2.1M), na mara 19 ya idadi ya uwanja mkubwa zaidi duniani wa Rungrado, unaoketisha watu 114,00 uliopo Korea Kaskazini. Hivyo, mantiki inatuonesha kuwa wawakilishi ndio walihutubiwa na Musa nao walikuwa na dhamana ya kusimamia wanayoambiwa.
✍🏾 Pia kabla hatujaenda mbali itafaa kutoa ufafanuzi kidogo wa maneno yaliyotumiwa hapa na yale ambayo yanaonekana kufanana nayo:
▪Mausia/Wosia ( _charges_) – ni vitu vyote vinavyokuongoza katika namna sahihi.
▪Sheria ( _Commandments_) – Amri kumi za Mungu (Mfano Usizini).
▪Torati ( _Law_) – maelekezo ya masuala mbalimbali (Sheria ya Zaka, Sheria ya Kafara, Sheria ya mirathi).
▪Amri ( _Statutes_) – ni kanuni za sheria, ni maelekezo yanayobainisha namna ya kutunza sheria (anayeishi na mtaliki wa mtu amezini, anayemwangalia mwanamke kwa kumtamani amezini).
▪Hukumu ( _Judgements_) – Uamuzi wa kuchukua pale amri zinapokiukwa (Mzinzi kupigwa mawe mpaka kufa).
Naamini ufafanuzi huu mfupi unaweza kukusaidia msomaji kuelewa jambo litakalokuwa limekusudiwa pindi ukutanapo na maneno haya wakati mwingine.
✍🏾 Musa katika hotuba hii anawakumbusha tena namna Mungu wao alivyowafanyia makuu ambayo _macho yao yameona,_ na hata mataifa yote wanakiri. Bwana anawatendea mambo hayo makubwa kwa namna 7 (fungu la 34):
▪ _kwa majaribu:_ - Bwana aliwajaribu kujenga imani yao kwake.
▪ _kwa ishara:_ - kama nguzo ya moto usiku na nguzo ya wingu mchana.
▪ _kwa maajabu:_ - kuonesha mkutano juu ya uweza na nia Yake.
▪ _kwa vita:_ - vita dhidi ya maadui wao, Waamori, Wamidiani n.k. na Bwana alivyowapigania.
▪ _kwa mkono hodari:_ - mkono wenye nguvu na uwezo usioshindwa.
▪ _kwa mkono ulionyoshwa:_ - namna Bwana alivyowatangulia katika mfululizo wa matukio.
▪ _kwa maogofya makuu:_ - mapigo kumi ya Misri.
✍🏾 Musa anawaonesha Israeli kuwa ushahidi walionao mbele yao ni mkubwa mno kutomtii Bwana. Endapo kizazi hiki kingekuwa na mashaka huu ni uthibitisho kuwa Mungu habadiliki, ni mshika maagano na mwaminifu. Aliwaahidi baba wa baba zao, akatenda kwa baba zao, atatenda pia na kwao. Musa anawausia ya kuwa endapo _hawatoongeza_ wala _kupunguza,_ sheria hiyo wosia hizo zitawafanya wao kuwa watu tofauti. Watakuwa ni watu wenye _*hekima na akili.*_ Mataifa yote yatawashangaa kwa namna watakavyokuwa na ustawi mkubwa.
✍🏾 Lakini endapo wangeenda kinyume, shida zingewaandama, kwa kuwa Bwana ni Mungu mwenye wivu. Endapo wangeasi, wangetawanyika, wangepungue idadi, wangekuwa watumwa, wangekuwa mateka na wangeangamia.
✍🏾 Katika hayo yote Musa anakusudia kuwaonesha watu umuhimu wa kutunza kumbukumbu wa yale ambayo Mungu amewatendea. kwa sababu katika hizo watamjua na wataweza kumtii Mungu wao. Ili kuwalinda na watoto wao pia ingewapasa kuwasimulia matendo makuu ya Bwana ili nao wawe na ufahamu wa huyu Mungu wao.
✍🏾 Na endapo wangekengeuka na kumwasi Bwana na _”kupatwa na mambo haya yote,”_ nao _”wakimtafuta Bwana, Mungu wao, watampata, wakimtafuta kwa moyo wao wote, na roho yao yote…..kwa kuwa Bwana, Mungu wao, ni Mungu wa rehema; hatakukosa wala kukuangamiza, wala hatalisahau agano la baba zako alilowaapia.”_
*Masomo:*
📍Kuweza kumtii Bwana inatupasa kufahamu nini anahitaji kwetu, yaani neno lake ambalo ndio kweli itakasayo (Yohana 17:17)
📍Kumpenda mpenzi wako kunahitaji uaminifu wa kiapo. Tahadhari na bidii kubwa inahitajika kujilinda dhidi ya majaribu ili kulinda uaminifu. Kudumisha upendo, daima inakubidi kurejesha kumbukumbu njema na kutengeneza nyingine tamu za safari yenu
Post A Comment:
0 comments: