Kumbukumbu la Torati 3

✒ Baada ya kumpiga mfalme Sihoni mfalme Ogu wa Bashani akapatwa hofu kuona kile Israeli ilichomfanyia mshirika wake. Mfalme Ogu ambaye ufalme wake ulikuwa na miji 60 yenye maboma marefu, ngome, malango na makomeo imara,pamoja na miji mingine mingi, aliamua kutoka kwenda kupigana na Israeli nje. Lakini, kwanini aamue kutoka kwenye miji hiyo imara akapigane nje?


✒ Jiografia ya Edrei inaonesha ilikuwa ni eneo tambarare iliokuwa katika mwinuko. Njia pekee ya kufika hapo ilikuwa ni nyembamba na ya mwinuko mkali, iliyojawa miamba ya volcano. Uchaguzi huo pia ulizingatia kuwa endapo wangeelemewa ingewawia rahisi kutokomea kwenye nyika ya miamba mingi iliyokuwa karibu ambayo ingekuwa ngumu kwa wageni kuweza kuwafata. Hivyo, mfalme Ogu alikusanya jeshi kubwa la kutosha tayari kwa vita hii. Kijeshi walikuwa wamechagua eneo zuri na la kimkakati kumkabili adui ambaye kwa matokeo yake alikuwa anatisha, lakini kwa mwonekano wake ni dhaifu.

✒ Mfalme Ogu alikuwa ni Mrefai (jamii ya majitu) aliyebakia katika eneo hilo. Kitanda chake kilikuwa ni cha chuma chenye urefu wa futi 12.5 (3.8m) na upana wa futi 6 (1.8m). Tukichukulia kwamba huenda kitanda kilikuwa kikubwa kumzidi na kusema labda alikuwa na urefu wa 3m tu, urefu huo bado ni wa kutisha. Rekodi ya mtu mrefu kwa ulimwengu wa sasa ni ya Robert Wardlov (1918-1940) wa Marekani aliyekuwa na urefu wa 2.72m, na mtu mrefu aliye hai leo ni Sultan Kosen wa Uturuki, mwenye urefu wa 2.5m. Hao wote hawakumfikia mfalme Ogu na jamii ya watu wake. Mwonekano wao ulikuwa ni wa kutisha bila shaka, haswa wakiwa wamebeba silaha. Kwa isivyo bahati kwao siku yao ilikuwa imewadia.

✒ Bwana akamwambia Musa _” Usimwogope; kwa kuwa nimemtia mkononi mwako, yeye na watu wake wote na nchi yake; nawe utamtenda mfano wa ulivyomtenda Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni”_ Musa alipowatia moyo watu wake na kuwaeleza ya kuwa Bwana atamfanya Ogu kama alivyomtenda Sihoni, hofu yao ikatoweka juu ya majitu haya na matumaini yao yakaelekea mbinguni, wakakumbuka ahadi zake na uaminifu wake Bwana.

✒ Israeli ikampiga mfalme Ogu na watu wake wote kwa uweza wa Bwana. Ikatwaa miji yake ya maboma 60 na mingine mingi. Wakawaua watu wote waume kwa wake na watoto, na mifugo yao wakaichukua nyara, huo ukawa mwisho wa wafalme wawili hawa wa Waamori Sihoni na Ogu.

✒ Maeneo haya waliyoyatwaa ya ng’ambo ya Yordani ndio yaliyogawiwa kwa makabila ya Gad, Reuben na nusu ya kabila la Manase. Nao kabila la Manase kwa kuwa walikuwa ni watu wa vita, walizidi kupanua mipaka yao.
Makabila haya yaliyopewa ardhi ng’ambo ya Mashariki mwa Yordani yalikula kiapo cha kutokuwa na makazi ya kudumu mpaka pale watakapomaliza kuwasaidia ndugu zao nao kutwaa sehemu za ardhi zao katika nchi ya ahadi. Ni katika maboma ya miji waliyoteka ndipo zilipoishi familia zao na mifugo yao huku wao wakiendelea kushika silaha kusaidia ndugu zao.

✒ Simulizi zote hizi Musa aliwasimulia wakiwa wamebakiza hatua ya kuvuka mto Yordani tu na kuingia nchi ya ahadi. Aliwaelezea pia namna ambavyo ilivyokuwa shauku yake na yeye aingie nchi hiyo na namna ambavyo alijaribu kumsihi Bwana amruhusu, bila mafanikio. Bwana alimkatalia na kumwomba asimwombe tena jambo hilo. Hapo awali Bwana alikuwa amemweleza Musa kuwa asingeingia nchi ya ahadi kutokana na yeye (Musa) kumkosea huko Meriba pale mkutano ulipolalamika.

✒ Bwana akamwambia apande mlima ili aweze kuitazama hiyo nchi ya ahadi. Kubwa zaidi Bwana alimwambia amuandae Yoshua aliyekuwa anaenda kuwa mrithi wake katika kuwavusha Waisraeli kuingia nchi ya ahadi.

*Masomo*

🔅 Inasikitisha kuwa sura ya 3 inazungumzia tu sifa ya ukubwa wa kitanda cha mfalme Ogu. Maria Teresa wa Calcutta ingawa alikuwa sista, mzee, dhaifu na mfupi, jina lake linaishi kwa namna alivyojitoa kuhudumia maskini, yatima na wahitaji. Malala Yousafzai mwaka 2012 akiwa binti wa miaka 15 alipigwa risasi na Taliban kwa kuwa mtetezi wa wanawake na watoto na kumfanya apate tuzo mbalimbali za amani ikiwemo ya Nobel mwaka 2014. Steve Hawkings (1942-2018) alikuwa mlemavu aliyekuwa hawezi kutembea, kuongea wala kufanya choc
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: