Agano ni makubaliano baina ya pande kuu mbili. Makubaliano haya yanakuwa yana common interest ndani yake au kitu ambacho wote wawili mnakuwa mnakitaka.
Agano ni tofauti na mkataba.Mkataba unaweza ukawa na maandishi tu au maneno ambayo yanakuwa na ushahidi wa watu wengine
Lakini agano halipo ivyo.Maagano yapo ya aina 2 tu
1.maagano kati ya wanadamu
2. Maagano kati ya wanadamu na Mungu
Kimsingi maagano haya mawili yananguvu sana. Unapoingia kwenye agano la aina yeyote,uwe na uhakika..kuna gharama kama utavunja hilo agan
Mfano agano la Ndoa.
Agano kama agano (lililokamilika) lazima lihusishe damu
Damu ya wanyama au wadudu,damu ya mtu nk
Damu ndiyo inayobeba uhai wa kiumbe chochote.
Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.
LAW. 17:11
Kwahiyo unapofanya agano uwe na uhakika unahusisha maisha yako kwa namna moja au nyingie kwa sababu damu yako imehusika.
Be very careful then
Hapo zamani hasa maeneo ya asia na ulaya kusini na sehemu baadhi za afrika,watu walikuwa wanafanya sana maagano ya damu na hata sasa bado baadhi ya sehemu yanaendelea
Nakumbuka mfano mmoja alitoa pastor benny hinn.
Akasema,wakati alipokuwa mdogo,familia yao ilikuwa na urafiki na familia fulani ya jirani yao,kiasi kwamba baba yake benny hinn alikuwa kama mmilik halali wa nyumba hiyo ya jirani,vivyo hivyo na baba wa nyumba iyo nyingine
Urafiki wao ulishibana sana mpka ikafika siku wazee hawa wawili wa hizi nyumba wakaamua kufanya agano anajiri ya familia zao.
Yakuwa,ikitokea mmoja kati yao anashida au amefariki,basi anayebakia anakuwa na majukumu yote kwa familia iliyobaki.
Benny hinn anasema,wakajikata kwenye vidole vyao,wakatamka hayo maneno niliyoandika hapo juu,halafu wakagusanisha viganja vyao ili damu zibadilishane,na damu kidogo wakaweka kwenye vikombe vyao vya vinywaji tofaut tofauti halafu wakanywa wote wawili.
: Agano likakamilika hapo.
Utagundua kuwa walifanya mambo matatu.
1. Makubaliano/agreements au ahadi
- Yakuwa tufanye hivi na hivi
2. Taratibu za agano (parameters)..sheria za agano
Walipokuwa wanagusanisha damu zao,kuna maneno walitamka ya kuwa,ataevunja agano hili mabaya mengi yamkute kati yake na familia yake.
3. Alama ya agano(sign and seal of the covenant)
Hii ndiyo damu iliyomwagika pale kama ishara ya agano
Mara nyingi agano la damu likifanyika,lazima kovu libakie (sijajua kwann).
Kawaida kila kidonda hupona na makovu hupotea,ila kidonda cha agano kovu lake halipotei na linaitwa SCAR OF THE COVENANT.
Kumbuka Yesu alipofufuka na kumtokea tomaso,alimwambia shika makovu yangu uone kama is sio mimi...yale ni makovu ya agano,hayafutiki...nakuambia mpaka Unyakuo utakapofika,bado Yesu atakuwa na yale makovu ya agano.
Namatumaini mpaka hapo umepata mwanga kidog juu ya maagano ya damu..
Kuna sehemu nataka nikupeleke na naamini tutafika na utaelewa umuhimu na kazi ya agano kwenye maisha yako
Tutaendelea wapendwa😰
Post A Comment:
0 comments: