(HAKUNA NAMNAπŸ˜ͺπŸ˜ͺ ITS TOO LATE). 

Dah inauma Sana usisome kama una moyo mdogo. 

Kuna ombaomba mmoja alikuwa anapenda kupita kwenye nyumba moja kila siku Ili kuomba chochote kitu kwaajili ya kuendesha maisha yake..

Omba omba nae ni mtu

 

Lakini yule mama hakuwa na moyo wa kumsaidia yule ombaomba Ila alikuwa anampa chakula kutokana na shinikizo la mumewe.

Siku moja yule mama baada ya kuona yule ombaomba amekuwa kero kwake aliamua kumuwekea sumu! Kwenye chakula Ili afe na asiendelee kumsumbua Tena 😒😒

Kweli mda si mrefu yule ombaomba alikuja na kubisha hodi!!! 

Siku hiyo Yule mama alikuwa ameandaa chapati," mixer na mayai. 

Mumewe akiwa hajui chochote kinachoendelea  alimwambia mkewe:-

We!  Mama JESE!?  fanya haraka umuandalie ndugu yetu chakula Ili Nayeye apate kula.

Yule mama akaandaa chapati 4 alizoziweka sumu Kali na kumfungia yule ombaomba kwenye mfuko na kumwambia nenda kale mbele ya Safari. 

Yule ombaomba alifurahi Sana kupewa chapati zile, bila ya kujuwa kuwa zilikuw na sumu Kali ndani yake. 😣😣

Ilikuwa ni mishale ya asubuhi yule ombaomba Alijisemea mwenyewe akiwa njiani! HIZI CHAPATI SIZILI SASA HIVI MAANA NITASIKIA NJAA MAPEMA ACHA NIZITUNZE HADI JIONI! 


********************************* 

Mida ya saa SITA mchana 12:25am

yule ombaomba akiwa kwenye pilikapilika zake Za kutangatanga mtaani aliona Watu watatu kichochoroni wamempiga roba yule mama anayempaga chakula πŸ’ͺπŸ’ͺ

Alitoka mbiyo Ili kwenda kumsaidia

WALE VIBAKA WALIVYOONA MTU WA AJABU ANAWAFATA MBIYO HUKU AKIWA AMEVAA MAVAZI YA AJABUAJABU WALIMUACHIA YULE MAMA NA KUKIMBIA.

Yule mama alivyoachiwa alianguka chini na kupoteza fahamu kutokana na Ile kabali Kari aliyopigwa. 

Yule ombaomba alisikitika Sana na kuamua kum'beba na kumkimbiza hospital πŸ™€πŸ˜”

Alipofika pale maness walimpokea na kuanza kumpa huduma ya kwanza. 

Yule ombaomba alitoa chapati 2 Kati ya zile nne zenye sumu na kuwaachia madocta na kuwaambia mgonjwa wangu akizinduka mpatieni hizi chapati ale Ili apate nguvu😭😭😭😭😭

Akawaachia kwenye ule mfuko na zile 2 zilizosalia akaondoka nazo Ili akazile mwenyewe

Yule mama alivyozinduka akapewa zile chapati ale!! 

Lakini alivyoona ule mfuko alishtuka Sana! 😱 na kuwaauliza maness hizi chapati ameleta Nani? 

Maness wakamwambia amekuachia mtu aliyekubeba na kukuleta hapa hospital Wakati Ukiwa hujitambui!! 😡

AKAULIZA YUPOJE? 

maness wakamwambia alikuwa amevaa nguo chafuchafu!! 

Yule mama akatambua kuwa alikuwa ni yule ombaomba na zile chapati ni zile alizoziweka sumu Alilia Sana 😭😭😭

Roho ilimuuma Sana na kujutia uamuzi wa kipuuzi aliyoufanya. 

Ikabidi atoke mbiyo pale hospital Ili amuwahi yule ombaomba kabla hajazila zile chapati Ili ampokonye.

Alimtafuta Sana na Mwishowe akaona Watu wengi Wanakimbilia dampo! 

Ilibidi Nayeye Aende kuangalia Kuna nini kinachoendelea!!!!! 

ALIPOFIKA PALE HAKUAMINI MACHO YAKE BAADA YA KUMUONA YULE OMBAOMBA AMESHIKA KIPANDE CHA CHAPATI MKONONI HUKU AKIWA AMEKUFA TAYARI😭😭😭😭😭

ALIKUWA AMESHACHELEWA!!!!!!!!!!! 

😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭

FANYA HARAKA KUYAFUTA MAKOSA YAKO KABLA HAYAJASABABISHA MAAFA KWA ULIYOWAKOSEA. 

MUNGU AKUONGOZE NA KUKUWEKA KATIKA NJIA ILIYONYOOKA...!

 Amen!πŸ™

Usisahau ku SHARE na wengine


Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: