A BOOK OF KNOWLEDGE FOR MAN AND WOMAN - A LOVE STORY FOR YOUTH (EPISODE 1), MAANA YA NDOA NA CHIMBUKO LA NDOA Biblia inasema, Hapo mwanzo Mungu aliziumba nchi na mbingu, pamoja vitu vyote tunavyoviona leo hii na vile tusivyoviona kwa haya macho ya nyama. Ikiwemo milima, mapepo, malaika, miti, wadudu, binadamu, majini na hata shetani mwenyewe.Vyote hivi ni kazi ya mikono ya Baba yetu aliye Mbinguni.
Dunia inaenda kwa kasi sana, na maisha ya mwanadamu kadri siku zinavyozidi kwenda mbele maisha yake yanazidi kurudi nyuma kimaarifa.Watu wengi sasa hivi wanaamini kuwa ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia ndio suluhisho la kila kitu,kitu ambacho sio sahii. Suluhisho la kila kitu ni Mungu, na pale tunapokwama lazima tumfuate Mungu ali atupe original formula zake na default settings za maisha kama yeye anavyotaka yawe.

Leo nataka tuangalie kwa ufupi moja ya kitengo cha Muhimu sana duniani na mbinguni kinachoitwa Ndoa na mahusiano.Ikumbukwe kuwa familia ndiyo chanzo cha mtaa,ukoo,jamii fulani na dunia nzima.Kila kitu unachokiona leo kimeanzia kwenye familia moja,kama ni kizuri au kibaya na chanzo cha familia ni ndoa,hii ndiyo deafult setting ya Mungu.Jamii inapoharibika,maasi yanapozidi au chochote kibaya unachokiona leo,basi uwe na uhakika chimbuko lake lipo kwenye ndoa.


Basi tuungane pamoja tunapoenda kuchambua chanzo hiki cha familia duniani.



MAANA YA NDOA NA CHIMBUKO LA NDOA

Biblia inasema, Hapo mwanzo Mungu aliziumba nchi na mbingu, pamoja vitu vyote tunavyoviona leo hii na vile tusivyoviona kwa haya macho ya nyama. Ikiwemo milima, mapepo, malaika, miti, wadudu, binadamu, majini na hata shetani mwenyewe.Vyote hivi ni kazi ya mikono ya Baba yetu aliye Mbinguni. 

(MWANZO 1:1-31)
 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni viti vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.”  (WAKOLOSAI 1:16).

Katika maandiko hapo juu, tunaona kuwa kila kitu alichokiumba Mungu kilikuwa safi na aliumba kila kitu (vinavyoonekana na visivyoonekana) kwa ajiri yake. - (MWANZO 1:31).

Mungu alimfanya mwanadamu (Mume) kwa mavumbi ya ardhi na akamuweka katika bustani aliyoifanya mashariki mwa  Edeni ambayo tayari Mungu alikuwa ameshaweka kila kitu ikiwemo na chakula ambacho Adamu anatakiwa ale na kumuagiza mwanadamu huyo atawale mahali pale bila kusahau kusudi kubwa la kuumbwa (kwa ajiri ya Mungu) kumuabudu Mungu Baba. - (MWANZO 2:7-9).

Tunaweza sasa kuanza kutazama chanzo cha ndoa kilikuwa ni kipi.
“Mungu ndiye chanzo halisi cha ndoa hii ya kwanza.”



MAANA YA NDOA KAMA AGANO
Ndoa ni muunganiko (fusion na sio bond) kati ya mwanamke na mwanaume ambayo hushuhudiwa na watu na Mungu akiwa shahidi wa agano hilo. (MALAKI 2:14).Agano kibiblia ni makubaliano kati ya pande kuu mbili, yaani Mungu baba na watu wake (wanadamu) ambayo hayawezi kuvunjika kwa njia yeyote ile.Makubaliano ya kiagano mara nyingi Mungu hutumia damu kuyathibitisha .Mfano
      I.        Agano la damu kati ya ibrahimu na Mungu
     II.        Agano la Damu kati waisraeli na Mungu enzi za mussa.
   III.        Agano la damu kati ya Mungu na Daudi.
   IV.        Agano la damu kati ya Mungu na Nuhu.
     V.        Na agano la mwisho na kubwa kuliko lote ni agano la Yesu pia kwa njia ya Damu.

Hapo mwanzo katika uumbaji wa Mungu, kila kitu  alichokiumba alikiona kuwa ni chema machoni pake,kuanzia uumbaji wa dunia mpaka wanyama wa mwitu.Lakini ni kitu kimoja tu Mungu ndio alichokiona kuwa sio kizuri      (NOT GOOD),ni Adamu kuwa peke yake.

“BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye” – (MWANZO 2:18-25).

Katika mistari hii, kuna neno ambalo limebeba ujumbe huu ambalo linasema
“SI VEMA” “IT IS NOT GOOD” adamu kuwa peke yake.Hapa Mungu aliona
kuwa kuna kitu kimepungua kwa Adamu,aliona kuwa adamu bado ana hitaji
ukamilisho fulani ili aweze kutimiza mapenzi ya Mungu au kazi ambayo
Mungu alikuwa amempa aifanye.Ndipo Mungu akasema “nitamfanyia adamu
msaidizi wa kufanana naye,ambaye ni mwanamke ,ili ndiye akawe
ukamilifu wa Adamu.

Mungu sasa akamfanya mwanamke ilia aje kuwa mke na msaidizi wa adamu (hapa ndipo kwenye matatizo hasa kwa wanawake).Hiki ndicho kilikuwa chanzo cha ndoa.Mungu ndiye aliyekuwa muanzilishi wa ndoa hii ya kwanza, au asasi hii inayoitwa ndoa, kwa kumtwalia Adamu mke na kumpa maelekezo ni jinsi gani ndoa yake itakuwa.
Adamu hakujitafutia mwenyewe mke, ila Mungu alitafuta mke ambaye ni sawa na kazi na Mapungufu ya Adamu ndipo akamletea.pia ndiye mtu pekee ambaye Mungu alimletea mke.

Bila Mungu kuona mapungufu kwa adamu basi uwe na uhakika ndoa isingekuwapo.
Kumbe kazi alizoumbiwa mwanamke ili aje kumkamilisha mwanamme zilikuwa mbili kama ifuatavyo.

 1. MKE (COMPANION)
Maana ya kwanza ya Mungu kumuumba mwanamke ni ili aje kuwa mke kwa Adamu na kutimiza unabii wa Mungu wa kuja kuijaza Dunia.Mke ni rafiki (companion).Mke ni muingiliano wa kiroho (agano) na ndio maana Adamu akasema “Mwanamme atawaacha wazazi wake naye ataenda kuwa mwili mmoja na mkewe” – hii ipo kiroho Zaidi.Unapooa au unapoolewa unakuwa mwili mmoja (kiroho) na mmeo au mkeo.Ndivyo maandiko yanavyosema.
MATHAYO 19:5,1KORINTHO 6:16, WAEFESO 5:31-33.

Kuna vitu vingi sana watu tunavichanganya juu ya ndoa. Inabidi tutambue kuwa lengo la kwanza la Mungu kumuumba Eva (mke wa adamu) haikuwa kuijaza dunia/kuwa na watoto, hashaa, ingawa ukisoma (MWANZO 1:28) maelekezo ya Mungu ni kuwa wazae na waijaze nchi.Lakini hii kuzaa na kuijaza nchi ni kazi ya ndoa lakini sio kusudi la Mungu kumpa Adamu mke.

Kusudi kubwa la Mungu kumuumbia mwanamke  Adamu ilikuwa ni kumuondolea upweke,Eva alikuja kuwa kampani kwa adamu,na ndio maana Mungu akasema “Sio vema mtu huyu awe peke yake”-maana yake sio vizuri huyu mtu awe mpweke.

Muinjilisti mmoja kutoka Bahama ,hayati myles munroe,anatafsiri ndoa kama COMPANIONSHIP COVENANT akimaanisha agano la urafiki kati ya mwanamke na mwanamme.Hii inamaanisha ndoa ni Zaidi ya kuwa na watoto,na neno mke lina maana Zaidi ya kuwa mama wa watoto.

Itaendelea ........... 
Weka maoni yako chini kwenye comment...

Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: