Baada ya kujua historia fupi ya Lucifer ama shetani ,leo tunaangalia tena kwa sehemu juu ya anguko la Lucifer
ANGUKO LA LUCIFER
Hadithii hii ya Lucifer inapatikana kwenye vitabi viwili vya agano la kale yaani Ezekiel 28 na Isaya 14.Ngoja tuchambue kimoja baada ya kingine kwa ufupi.
Hadithii hii ya Lucifer inapatikana kwenye vitabi viwili vya agano la kale yaani Ezekiel 28 na Isaya 14.Ngoja tuchambue kimoja baada ya kingine kwa ufupi.
Katika Ezekiel 28,mistari kumi ya mwanzo inamuelezea mkuu wa Tiro ama mfalme wa mji wa Tiro ambaye biblia inamfananisha na shetani na waandishi wengine wanasema alikuwa shetani mwenyewe akiuongoza mji huo na kuanzia mstari wa kumi na moja tunaona sasa habari ikihamia kwa Lucifer ama shetani.
Mistari hii ina maana gani? Katika hii mistari 10 ya mwanzo biblia inamzungumzia mfalme wa Tiro ambaye alijitia uungu wakati yeye ni mwanadamu,Baadhi ya waandishi wanasema,japokuwa aliyekuwa mfalme anayeiongoza Tiro ni mwanadamu lakini kiongozi sahihi au kiongozi mwenyewe au mfalme mkuu wa Tiro alikuwa ibilisi/Shetani mwenyewe.
Pia wengine wanaamini kuwa mistari hii inamzungumzia mfalme wa tiro ambaye alikuwa empowered/alipewa nguvu na shetani.
Sasa kuna vitu vya kweli juu ya mfalme wa tiro ambavyo anatueleza nabii ezekiel ambavyo ukiviangalia utajua kuwa mfalme huyu wa Tiro/Tyra hakuwa mwanadamu wa kawaida kama mimi na wewe.
1. ASILI YAKE
katika ezekiel 28:14 maandiko yanamzungumzia mfalme wa Tiro kama Kerubi aliyetiwa mafuta afunikaye. Hawa makerubi au (Cherub) kwa kiingereza ni malaika wa kiwango cha juu sana mbinguni.Sasa tunaona mungu anamtaja mfalme wa Tiro kuwa kama mmoja wa makerubi tena aliyepakwa mafuta tena afunikaye akiwa na maana mlinzi pia.

2.UKAMILIFU WAKE
Katika msatri wa 15 hapa biblia inamuelezea kuwa alikuwa mkamilifu sana Tangu alipoumbwa mpaka pale uovu ulipoonekana ndani yake. Tunajua kuwa hakuna mwanadamu ambaye ni mkamilifu mbele za mungu Tangu adamu.

3.ALIKUWA NA CHEO CHA KIPEKEE
Hii inaonekana katika mstari wa 14 na 15 ambako maandiko yanasema "Nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa mungu" Je ni mwanadamu gani ambaye mungu amemuweka kwenye mlima wake?
Hii inaonekana katika mstari wa 14 na 15 ambako maandiko yanasema "Nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa mungu" Je ni mwanadamu gani ambaye mungu amemuweka kwenye mlima wake?
4.AFUKUZWA KWENYE MLIMA WA MOTO
Katika mstari wa 16 baada ya udhalimu kuonekana ndani yake mungu anaamua kumfukuza kutoka katika ule mlima na mawe ya moto na kumuangamiza.
Katika mstari wa 16 baada ya udhalimu kuonekana ndani yake mungu anaamua kumfukuza kutoka katika ule mlima na mawe ya moto na kumuangamiza.
Kwa sifa hizi unaweza kujua kuwa nabii Ezekiel alikuwa hamzungumzii mwanadamu wa kawaida bali shetani mwenyewe. ukipitia mstari wa 12 mwanadamu anaagizwa amfanyie maombolezo mfalme wa Tiro kwa kuwa alikuwa amejaa Hekima,ukamilifu wa uzuri,alikuwa ndani ya Eden bustani ya mungu na Filimbi pia zilikuwa ndani yake.dhahiri hapa tunaona kuwa mfalme wa Tiro alikuwa Shetani mwenyewe.
Maandiko haya ya Ezekiel 28:12-15 yanaeleza kuwa mfalme wa Tiro alikuwa kiumbe akiyeumbwa na mungu na akipewa ukamilifu katika kila eneo na alibaki katika hali iyo ya ukamilifu mpaka pale dhambi ilipoonekana kwake.
je,ni dhambi gani hii?
17,katika mstari wa 17 unaweza kuona dhambi iliyomfanya mungu amtekeketeze na kumtoa mfalme huyo wa Tiro katika milki yake.Lucifer ama shetani alidanganya na uzuri wake,ukamilifu wake pamoja na cheo chake mpaka ikampelekea kuutaka utukufu wa Mungu mkuu.Kwa hiyo dhambi pekee iliyomuangusha shetani ilikiwa ni kiburi na baada ya kutupwa mpaka nchi,dhambii hii hii ya kiburi ndiyo ikawa dhambi ya kwanza kuingia ulimwenguni na kuwameza adamu na Hawa. Mwanzo 3-19.

Na huu ndo ulikuwa mwanzo wa dhambi ulimwenguni. Ezekiel 28:18
Maandiko hayo hayamaanishi shetani hakuwa na uhuru au access ya kuingia mbinguni tena.... Katika sehemu ijayo tutaangalia swala hilo pamoja na Ufalme wa Tiro.Mungu akubariki
aweosme
ReplyDelete