Leo tuataanza kuangalia sababu zilizomfanya shetani ashushwe kutoka mbinguni mpaka nchi (Duniani) ilihali hapo zamani alikuwa mbinguni na alipewa jina kubwa sana kama Nyota ya asubuhi ama Lucifer kwa maana nyingine..
Siku ingine tutakuja kuona jinsi sekretarieti au uongozi wa mbinguni ulivyokuwa.Lakini leo tuangalie maandiko machache tu ya jinsi shetani alivyoondolewa mbinguni na mungu mwenyewe,tutaangalia na dhambi gani ilifanyika mbinguni ambayo ilisababisha shetani au lucifer atupwe..
Haya maandiko yanaonesha jinsi alivyoondolewa mbinguni
isaya 14:12
"Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajirimwana wa asubuhiJinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!"
Kwenye maandiko hayo kuna mambo tunajifunza kama mawili hivi
1.Lucifer  mwana wa asubuhi
2.Lucifer kama shetani
1.LUCIFER MWANA WA ASUBUHI
Lucifer ni neno la kiebrania lenye maana ya Mwangaza wa asubuhi .kwa lugha nyingine ni sayari ya Venus ambayo mwangaza wake uonekana asubuhi .
Je ni Kweli lucifer ni kiumbe kilichoumbwa ??
Ikumbukwe kuwa maandiko matakatifu yanatueleza kuwa Mungu ndiye muumba wa Kila kitu ,  waefeso 3:9 ......
Hii inaonyesha pia lucifer ni kiumbe kilichoumbwa na Mungu. 
Je wajua  lucifer alikuwa mwimbaji maarufu huko mbinguni. ..........? 
Lucifer alikuwa malaika mkuu wa sifa..
Mungu wetu ni Mungu anayependa kusifiwa maandiko yafuatayo yanaelezea vizuri jinsi Mungu ni wa sifa LUKA 19:37-40, ISAYA 42:8, ZABURI 111:10, MATENDO 3:8   Mungu wetu ni wa sifa na kazi hii ilifanywa kwa umahiri na ustadi mkubwa na lucifer.
ITAENDELEA. ..................
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

1 comments:

  1. Kuna tofauti kati ya nyota ya alfajiri na nyota ya asubuhi...pia Kuna tofauti kati ya lusifa na ibilisi.. lusifa ni nuru au mwangaza na ibilisi ni uovu au matendo mabaya ya sirini yaani matendo ya gizani

    ReplyDelete