Na 
Mwl. Anna Mwidete 
0754623278/0715623278

Salam ndugu zangu,Nawapenda sana. 
Mimi ni mtumishi wa Mungu,nimeokoka na Yesu ni Bwana kwangu.Ni mama wa familia na nipo kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 20 sasa.Pia ni mwalimu mzuri sana wa ndoa/mahusiano na nimejikita sana kwa wanawake,ila hii haimaanishi kama wanaume hawanihusu,hasha.


Leo ni siku nyingine tena ambayo nimeona vyema kujifunza na nyinyi habari za ndoa na utaratibu wake. Mafundisho haya ni marefu kwa hiyo nitayagawa kwa vipande vipande.Kuwa huru kuuliza chochote kupitia komenti hapo chini au kwa simu.Karibu sana

Ndoa ni nini basi?
Ni makubaliano kati ya watu wawili tu,ambao kwa hiari yao na kwa viapo wameamua kuishi pamoja kama mke na mume kwenye mashine au mfumo unaoitwa ndoa.

Kwa sisi wakristo,watu hawa wawili wanakuwa wameingia kwenye agano,agano la ndoa kwa yale maneno tunayotamkaga yanayosema "kifo kitutenganishe". Pia ukumbuke,ndoa ilianzishwa na Mungu mwenyewe pale Eden kati ya Adam na Hawa.
MWANZO 2:21-24 NA MATHAYO 19:5.

Kama ni Mungu ndiye aliyeanzisha ndoa,basi aliweka taratibu na kanuni za  kuzifuata ili hawa wanandoa waishi kwa furaha na amani.Ndoa sio ndoano kwa Mungu.

Unaweza ukasoma vitabu vingi au ukafanya kila kinachofanyika lakini ukashindwa kumaliza migogoro iliyopo kwenye ndoa yako.

Ninakuambia,kama hatutafuata utaratibu aliouweka Mungu mwenyewe,matatizo ya kwenye ndoa hayawezi kuisha na tutabaki tunasema ndoa ni ndoano au ndoa ni bahati ya kuwa uvumilie tu. Mungu alianzisha taasisi hii sio kwa lengo la nyie wawili mvumiliane,ila alitaka muishi kwa amani na furaha milele.

1.Wengine wanaomba na kufunga lakini tatizo lipo pale pale.
2.wengine wanasema watakuwa wapole sana na kuongea kwa sauti za unyenyekevu,lakini tatizo lipo pale pale.
3.mwingine anashinda analia,lakini hakuna wakumuonea huruma

Yote hayo na mengine unayofanya ni bure mpendwa kama hujakaachini na kufuata utaratibu aliouweka Mungu ambaye ndiye injinia wa ndoa zetu....

WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA.

Kuna maarifa ya kufuata ili kuhakikisha ndoa zetu zinakuwa salama.Ndoa zisipokuwa salama basi hata taifa haliwezi kuwa salama hata kidogo.Lazima wewe kama mwanamke utafute namna ya kuiponya ndoa yako

Katika kipindi kinachofuata,tutatazama kwanundani

TARATIBU ZA MUNGU KWENYE TAASISI YA NDOA 

Masomo yangu yanapatikana kwenye tovuti ya

Tzworships.blogspot.com 

Nitafurahi kama nitaona komenti zako hapo ili na mimi nijifunze zaidi.

Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: